03/09/2026
LEO TUNAMZUNGUMZIA NAHODHA WA EMBE FC!
Peter Mugendi almaarufu CHAMPEE
Leo zamu ni ya kiungo wetu ambaye si tu anajua kupanga mipira, bali pia anajua kupanga watu!
Ni nahodha wa EMBE FC, mwenye ustaarabu wa hali ya juu—mpira ukipotea, hasemi “umeupoteza wapi?” Anaanza kwa kuuliza, “Tujipange upya ndugu zangu.”
Uwanjani ni mtu wa utulivu, hekima na nidhamu. Hata akikasirika, bado hasahau kuwa yeye ni nahodha…
Kiungo mahiri Nahodha mwenye heshima na Mtaalamu wa kupanga mchezo ni Mwenye ustaarabu wa kupigiwa mfano
Kwa kifupi, huyu ni nahodha ambaye anaongoza kwa miguu uwanjani na kwa busara nje ya uwanja!
EMBE FC: Heshima kwanza, mpira baadaye!