25/08/2026
Mwanamuziki ametangaza ujio wa Album yake 'Love Kingdom' ambayo itaachiwa rasmi mwisho wa mwezi huu Agosti 30!
Album yake hiyo itakuwa na nyimbo 19, imetengenezwa na ma-producer 6 tofauti na wasanii 11 wameshiriki Album yake.
Wasanii watakaosikika kwenye nyimbo za Album ni Belle9, Q Chief, Barakah The Prince, Mr Kesho, Foby, Steve Rnb, Dayoo, Kayumba, Luna Miguel, Back Vocalist na Nuruelly.