21/10/2024
SHABIKI wa Yanga unayeshangilia ushindi wa timu yako soma hii, namna mabosi wa klabu yako na kipa wenu Djigui Diarra alivyosafirishwa kimafia kuiwahi mechi dhidi ya Simba, akishuka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 3 na kufika uwanjani kisha akaibeba timu yako.
Kipa huyo juzi alitua uwanja wa ndege Dar es Salaam saa 8 mchana, kisha kwenda moja kwa moja Uwanja wa Benjamin Mkapa akiisubiri timu yake na kikosi kilipowasili saa 9 alasiri akaungana nacho na kufanya kazi ya kishujaa.
Iko hivi; Oktoba 15 Mali ilikuwa ugenini Guinea Bissau ikicheza mechi ya kuwania nafasi ya kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa Afrika, mechi iliyoisha kwa suluhu huku kipa huyo akiwa golini.
Baada ya mchezo huo, alilazimika kusubiri ndege maalum ya kuwarudisha Mali lakini baadaye ikachelewa huku kukiwa hakuna ndege nyingine kwa haraka.
Kipa huyo aliijulisha klabu yake haraka na msako wa kumleta nchini ukaanza na kupata nafasi moja pekee kwenye ndege inayotoka Guinea kwenda Senegal umbali wa kilometa 308 akitumia dakika 35 kufika.
Yanga ililazimika kumpeleka Senegal ikiwa ni taifa karibu na Guinea Bissau ambako angepanda ndege ya haraka ya kuunganisha
Hapo Senegal akapata ndege Oktoba 18 iliyompeleka hadi Dubai akisafiri umbali wa kilo meta 7640.04 alaunganisha ya kumleta Dar es Salaam.
Diarra k**a angechelewa kwa saa moja tu kufika Dubai, safari yake ingekwamia hapo kuwahi mechi ya Simba ambako alikuta tayari kuna maafisa wanamsubiri kumuwahisha kwenye ndege inayokuja nchini.
Kipa huyo akatumia saa 5:30 kusafiri kutoka Dubai hadi Dar es Salaam umbali wa kilometa 3999.23 akiwasili saa 8:00 mchana ambako nako alikuta watu wanamsubiri kuanzia ndani mpaka nje kumuwahisha uwanjani.
Diarra alitoka uwanjani hapo saa 8:20 mchana kisha kuwahishwa Uwanja wa Benjamin Mkapa akikuta hata wenzake hawajafika kutokea AVIC Town.
Mara baada ya kufika uwanjani, kipa huyo aliingizwa vyumbani na kuanza kutengenezwa kisaikolojia na mabosi wa Yanga kisha akawaambia yuko tayari kucheza mechi hiyo.
Ndani ya mchezo huo, Diarra hakuonyesha k**a ni kipa aliyekaribia kuukosa mchezo huo na dakika tano tu, akafanya kazi ya kibabe akiokoa majaribio mawili makubwa ya Simba