Dimba la Nyumbani

Dimba la Nyumbani Habari na matukio mbalimbali ya michezo

*Habari* Karibu Rasilimali Zetu Media – sauti ya utamaduni, habari na michezo!Hapa tunaleta habari za kina, sanaa za asi...
12/05/2025

*Habari*

Karibu Rasilimali Zetu Media – sauti ya utamaduni, habari na michezo!
Hapa tunaleta habari za kina, sanaa za asili zenye utamu wa asili, k**a vile mganda,Kioda,ngawa ,matuli, nyimbo za makabila mbalimbali na michezo inayoburudisha .

Kila video ni hazina ya maarifa, burudani, na uzalendo.

Ikiwa unapenda kuona uzuri wa utamaduni wetu uking’aa, habari zenye ukweli, na michezo ikipamba moto...

Basi usikose kufanya haya matatu muhimu:
Like, Subscribe, na Gonga kengele!

Tusaidie kusambaza ujumbe huu toka rasilimali zetu – maana hizi ni zetu sote!

Rasilimali Zetu Media – Tunahifadhi, tunahabarisha, tunaburudisha.

Tembelea kwenye link ifuatayo
https://youtube.com/?si=1WZyHosmuhswInWg

Asante Kwa wote

Rasilimali Zetu Plus TV ni kituo cha YouTube Na Social Media kinachojitolea kutoa elimu na taarifa kuhusu rasilimali asili, nishati, mazingira, na maendeleo endelevu. Tunatoa maarifa muhimu yanayosaidia jamii kuelewa umuhimu wa utunzaji wa rasilimali na kutafuta suluhisho za changamoto zinazohusiana...

Michezo Mbalimbali ambayo inatachezwa katika wilaya ya Ludewa Lengo ni kukuza na kuendeleza sekta ya michezo katika wila...
25/05/2024

Michezo Mbalimbali ambayo inatachezwa katika wilaya ya Ludewa Lengo ni kukuza na kuendeleza sekta ya michezo katika wilaya yetu kampeni hii inaendeshwa na Rafiki fm redio Ludewa

17/03/2024

SIMBA NA DAMU YA CLOVIS ACOSTA FERNANDES, TASWIRA YA O JOGO BONITO ROBO FAINALI AFRIKA 2019
Unamfahamu shabiki wa Brazil wakuitwa Clovis Acosta 'Gaucho da Copa' Aliesafiri nchi zaidi ya 60 kushuhudia mechi zaidi ya 150 za timu ya Taifa ya Brazil?? Mungu amlaze mahali pema, damu yake na spirit yake walikuwa nayo mashabiki wa Simba, usiku wa Machi 16,2019
Unaufahamu mchezo wa soka tamu na la kuvutia?? Napenda kuliita Freestyle football, Wareno wanaliita O Jogo Bonito, ndilo soka walilocheza Simba usiku ule dhidi ya AS Vita, falsafa yao ya siku zote Simbarcelona
Kuelekea usiku ule wa Kocha Patrick Aussems alikua anaenda kuingia kwenye daraja la Kocha Paul West Gwivaha huyu aliwapeleka Simba Nusu fainali Ligi ya Mabingwa 1974, aliku anaenda kujiweka daraja la Kibadeni Mputa na Enteneh Esheteh, hawa waliipeleka Simba fainali Shirikisho 1993
Nilitaka kumsahau Kocha Nabby Camara wa Guinea, mvumbuzi mkubwa wa vipaji 1975, Wazee wangu mnawakumbuka Abbas Kuka, George Best Kulagwa, Nico Njohole na Filbert Rubibira, nakumbuka usiku ule Aussems alituletea Rashid Juma 'Game Changer'
Binafsi Majira ya saa5 asubuhi kuelekea mechi ile nilisimama pembeni pale Ubungo Mataa, kushuhudia Wanasimba wakitiririka kwenye mabasi kuelekea Taifa, namkumbuka Traffic wa zamu akipata wakati mgumu kuruhusu magari kushika Mandela Road
Wakati naendelea kushangaa nilishuhudia Wahafidhina wa Ubungo wale wafia timu Wekundu wa Terminal wakijiandaa kuelekea Taifa, jezi zao za nakshi nakshi, majigambo yao na bendera mbele ya gari lao kuonesha ukubwa wa timu zao, kila mtu kauvaa uhusika
Ni mechi ya kisasi hii, ni mechi ambayo Haji Manara De Le Boss ameshatoa sumu za kutosha ni DO OR DIE, nilijishika tama na kuwatazama Wanyama wakiwa na vibe lao, nilipokumbuka miguu ya Francis Luamba Ngoma, Botuli Bompunga na Kazadi Kasengu nilizidi kushangaa
Lakini Mwanamama mmoja wakati nipo kwenye daladala kuelekea Taifa alikuwa anatoa darasa, alitukumbusha Ngurumo za Mnyama barani Afrika, alitukumbusha kichapo cha Zamalek na chupuchupu ya Stella Abdijan na Mehrar Kubra, aliamini Simba ni timu kubwa ya hatua kubwa
Vuvuzela zinapigwa njiani nami bado nipo kwenye tafakari kubwa, bado mawazo yangu nawaza zile bao 5-0 pale Congo ya Kinshasa, naikumbuka miguu ya Kazadi Kasengu, Ngoda Muzinga, Jean Makusu na ujuvi wa Fabrice Ngoma, bado naikumbuka Vita ilicheza fainali kombe la Shirikisho Afrika hapo nikazidi kuishiwa nguvu
Wakati nipo zangu jukwaa la buku tano, nimetulia kupitia kikosi cha Simba kilichomkosa Jonas Mkude, Aussems alikuja na 4-3-3 James Kotei "The Pitbull" na Mzamiru Yassin "Box to Box Midfielder" wakianza, Kiungo cha Vita wana Captain Nelson Munganga na Wangu Mbambu, nikizidi kupagawa
Bibi mmoja pembeni Mwenyeji wa Iringa huko Dabaga, aliniambia hii ni mechi kubwa lakini Simba tumeshawahi kufanya makubwa, Mg Will "sisi tulishinda kule Ivory Coast, sisi tulimvua ubingwa Zamalek, sisi tulimuangusha Ahly hapa Taifa, amini hii ni Simba, hapa tunatoka salama" alinipa moyo tu
Mechi imeanza, kwa kasi sana ila dakika ya 13 tu Kazadi Kasengu anaingia wavuni, lakini ajabu hakuna shabiki wa Simba alietulia, bado watu waliyaona maajabu ya 1993 na 2003, bado watu waliyaona maajabu ya Aussems k**a yale ya West Gwivaha, dakika ya 36 Beki ya kushoto MO Hussein kwenye box wamo🙌
Ile 1-1 ilizidi kuwaamsha Mashabiki, wakati huo namtazama Yule Bibi kutokea Dabaga, alirudi tena kuniambia "Yule Zimbwe ni k**a Mohamed Kajole Machela, aliwahi kupita Simba, wanafanana sana" nilianza kuingiwa na imaan, wakati huo Mashabiki wa Simba wameamsha mzuka jukwaani
Kipindi cha pili kimeanza ilimlazimu Aussems awe na akili nyingi alimtoa Immanuel Okwi na kumpa nafasi Haruna Niyonzima, Vita walijibu kwa kuwaleta Ducapel Moloko, Cesar Manzoki na Jeremie Mumbele, mpira ulianza kupigwa mwingi huku watu wakitazama matokeo ya Ahly dhidi ya JS Saoura
Bibi yule alinigeukia tena aliniambia "Maajabu ya Simba inahitajika Sub, k**a ya George Kulagwa 'Best' tunahitaji winga k**a yule, 1979 marudiano pale Zambia na wale Mufulira Wanderers alituwekea bao mbili kwenye ile comeback", Kocha atuletee winga ndani, Nilimuelewa tena wakati pira linapigwa jingi bado 1-1.
Dakika zikianza kucheza kwenye 70, huko Cairo National Al Ahly anaongoza 1-0 dhidi ya JS Saoura, bao walojifunga dakika ya 30 tu ya mchezo na Fateh Talah, huku mechi ya Simba ilikua lazima ashinde ili apite na sare ingembeba Vita
Dakika ya 78 anaingia Hassan Dilunga kuchukua nafasi ya Mzamiru Yassin, tena dakika ya 85 anatoka James Kotei anaingia Rashid Juma, niliwaza sana Simba hii sasa bila Kiungo Mkabaji, mbinu pekee ni kumiliki mpira na kushambulia ili wasishambuliwe
Wakati majukwaa yanaendelea kuamsha mizuka, nilitupa macho uwanjani, Mohamed Hussein na Zana Coulibaly wakawa wing backs kabisa, kisha nikamuona Haruna na Chama k**a Perfect 8s, ama double 8 wakifanya kazi ya kuwarudisha Vita nyuma
Ghafla nilitaka kujua Dilunga ana kazi gani, nikagundua anacheza k**a semi winger, Simba ikiwa kwenye transition ni 2-3-5🙌 huko pembeni Rashid Juma akicheza mzani sawa na Tshabalala kuwavuta Vita, mchezo wa hatari wa Space Exploitation
Bibi yule wa Dabaga alinitazama tena ila safari hii kwa tabasamu, alisema "Sasa tunaenda kuiona Simba ya 1979 pale dimba la Independence Lusaka" nilizidi kumuelewa, Simbarcelona wakaanza kuzihesabu pass, Sunderland Abijoo wanatakata, Haruna na mpira, Chama na akili kisha Rashid na kasi k**a ya Thuwen Ally
Kwenye ukuta Erasto Nyoni k**a George Magere Masatu na Pascal Wawa k**a Fikiri Magoso, ndipo hapa nilishuhudia O Jogo Bonito, falsafa yao Simba ya soka tamu, jukwaani MO Dewji anavuta uradi, Mashabiki juu juu, Jonas Mkude na mashabiki wanaliamsha sana, watu wamevua mashati
Niyonzima anapiga pass huku anamfundisha Chama wapi pakukaa wametawala Golden Square, mpira mmoja mrefu kutoka mikononi mwa Manula kwake Haruna pembeni anagonga grasscutter pass kwa Bocco aliyesogea pembeni, haraka sana Haruna na Chama ndani ya box
Bocco analeta pass kisha Haruna anafanya dummy play anaupisha mpira, dakika ya 89!Chama one touch, Chama second touch, far post goal🙌🙌🙌 kilichobaki ni historia, siku nyingine na comeback nyingine tena
Allez SIMBARCELONA🙏❤

*LIGI DARAJA LA NNE WILAYA YA LUDEWA KUANZA SEPTEMBA 2022*Na Njenje ze RopoLudewa NjombeChama Cha mpira wa miguu wilaya ...
17/08/2022

*LIGI DARAJA LA NNE WILAYA YA LUDEWA KUANZA SEPTEMBA 2022*

Na Njenje ze Ropo
Ludewa Njombe

Chama Cha mpira wa miguu wilaya ya Ludewa katika ratiba zake za maendeleo ya mpira wa miguu kwa wilaya wanatarajiwa kuandaa mashindano ya ligi ya wilaya ya Ludewa darajaa nne.

Ligi hiyo yanatarajiwa kuanza mwezi September mwishoni kwa kushirikisha timu zote za mpira wa miguu wilaya ya Ludewa.

Katibu wa chama Cha mpira Ludifa Ndug Fadhili Mhagama katika barua ya kuviomba vilabu kushiriki ametanabaisha kuwa vigezo vya kushiriki ni pamoja na kulipa Ada ya kiingilio Tsh.50000/= kwa kila timu shiriki.

Pia barua imeeleza kuwa Mwisho wa kulipa Ada ya ushiriki ni Tarehe 1.09.2022

Ligi hiyo inatarajiwa kufanyika kwa kanda zote sita za kimichezo Endapo timu zitajitokeza kwa wingi.

Ikumbukwe kuwa bingwa wa michuano atapata nafasi ya kwenda kushiriki ligi ya mkoa wa Njombe pamoja na Zawadi nyingine nyingi.

Ambapo mshindi wa kwanza atapokea kitita Cha pesa kisicho pungua laki tano ( Tsh.500000/=)
Sambamba na mshindi wa kwanza Hadi wa tatu.

Chama Cha mpira wilaya ya Ludewa kinaomba wadau wa michezo waweze kuchangia pale watapoguswa ili kuweza kujenga michezo imara ndani ya Ludewa pamoja na timu za mpira wa miguu zilizopo Ludewa.

(Unaombwa kushare ili ujumbe ufike kila sehemu)

Kwa mawasiliano zaidi

Habari na mawasiliano
0755666795

10/08/2022

*HATUA YA 16 BORA LIGI YA KUAMBIANA CUP*

11.08.2022
Sagulu fc vs kipingu fc

12.08.2022
Lihagule fc vs lake star

13.08.2022 saa 14.00

Shuma fc vs Ilela fc

13.08.2022 saa 16.00

Luilo fc vs Kingole fc

14.08.2022 saa 14.00

Kimelembe Fc vs mbongo fc

14.08.2022 saa 16.00

Mbande fc vs Nkomang'ombe fc

15.08.2022

Igalu fc vs kipangara fc

16.08.2022

Homeboys vs Masasi

*MICHEZO YA ROBO FAINALI*

17.08.2022
Mshindi
Kipingu/sagalu vs Lihagule/Lake star

18.08.2022
Mshindi
Shuma/Ilela vs Luilo/Kingole

19.08.2022
Mshindi

Kimelembe/Mbongo vs Mbande/Nkomang'ombe

20.08.2022
Mshindi

Igalu/Kipangara vs Homeboy/masasi

*NUSU FAINALI*

22.08.2022

*Nusu fainali ya kwanza*

Mshindi wa robo fainali ya kwanza vs mshindi wa robo fainali ya pili

24.08.2022

*Nusu fainali ya pili*

Mshindi wa robo fainali ya tatu vs mshindi wa robo fainali ya nne

26.08.2022

*Mshindi wa tatu*

Timu zilizopoteza mchezo wa Nusu fainali

27.08.2022
*Fainali*
Washindi wa nusu fainali

SHUMA YASHUSHA MVUA YA MAGOLI KWA WALIMA MPUNGA LIGI YA KUAMBIANA WILAYA YA LUDEWALigi ya kuambiana cup imeendelea kutim...
22/07/2022

SHUMA YASHUSHA MVUA YA MAGOLI KWA WALIMA MPUNGA LIGI YA KUAMBIANA WILAYA YA LUDEWA

Ligi ya kuambiana cup imeendelea kutimua vumbi hii leo katika uwanja wa masasi wilaya ya Ludewa mkoani Njombe .

Katika mchezo huo wa kundi c uliwakutanisha shuma kutoka Ngelenge dhidi ya walima mpunga wa lifua Nkinila.

Dakika 90 zilitosha kuwapa Ushindi timu ya Shuma kwa jumla ya magoli 6 kwa 0

Magoli ya Shuma yamefungwa na Chedi Mapunda Dk 10 na dk 57
Richard Haule dk 53 Richard Kimata dk 55 na dk 85 pamoja na Stephano Phadhili dk 80

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho katika uwanja wa masasi wilaya ya Ludewa kwa kuwakutanisha Igalu dhidi ya kipingu.

Chama Cha mpira wilaya ya Ludewa tunasogea karibu Yako zaidi Kwa maoni na ushauri karibu katika kundi la WhatsApp la mic...
15/06/2022

Chama Cha mpira wilaya ya Ludewa tunasogea karibu Yako zaidi Kwa maoni na ushauri karibu katika kundi la WhatsApp la michezo chama Cha mpira wilaya ya Ludewa lengo ni kujenga na kukuza michezo katika wilaya yetu ya Ludewa...

Gusa link hapa chini kujiunga nasi

https://chat.whatsapp.com/CQklpLKQ2rn6DFfkncqymq

Pia habari zetu utazipata kupitia kurasa ya Facebook inayoitwa chama Cha mpira wilaya ya Ludewa

Karibu sana

WhatsApp Group Invite

Kamonga league disivion 4 ludewa mgao wa zawadi ligi ya wilaya Ludewa .Kushiriki wa vilabu Pamoja na kikao Cha viongozi ...
25/11/2021

Kamonga league disivion 4 ludewa mgao wa zawadi ligi ya wilaya Ludewa .
Kushiriki wa vilabu
Pamoja na kikao Cha viongozi wa timu wanaopenda kushiriki ligi ya wilaya ya Ludewa sambaza taarifa hii Ili iwafikie wanamichezo wote Ludewa

Address

Ludewa
Njombe

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dimba la Nyumbani posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Dimba la Nyumbani:

Share