28/01/2022
“Nimejaribu kupiga story na Kiongozi mmoja ndani ya bench la Simba kuhusiana na hukumu ya Mwalimu Pablo, binafsi ilinifikirisha sana matukio ya kujirudia kwa mechi tatu”
“Kiongozi akaniambia wanakubali kuwa kwenye mechi ya Mbeya City pale Sokoine ni kweli hakuongea na Manungu dhidi ya Mtibwa pia hakuongea baada ya mechi”
“Ila mechi ya Kagera Sugar dhidi ya Simba baada ya mechi wakati wanahitaji Kocha azungumze, Simba wakawaambia atazungumza Kocha Mkuu Pablo kwakuwa ataelezea vyema na sio Kocha Msaidizi”
“Baadae Wahusika waliwaambia kuna shida ya lugha Hivyo wanaomba Matola aongee ila Kiongozi aliendelea kuwasisitiza kuwa kutokana na matokeo anaepaswa kuongea ni Head Coach kwakuwa ndie Mtu sahihi zaidi”
“Hivyo anadai Kocha Mkuu hakukataa kuongea baada ya mechi ya Kagera bali Wahusika walishindwana na Kiongozi Kuhusu nani aongee ikisemekana tatizo ni lugha”
“📌Hayo ni majibu ya Kiongozi baada ya Mimi kuhitaji kufahamu inawezekana vipi Simba wakaruhusu makosa ya 'rejareja' k**a haya”
“🚨KAMA TATIZO NI LUGHA, JE NI KOSA LA NANI?”
- Ameandika Jr