08/06/2024
✍🏿✍️Vyombo vya habari vya Uingereza Kila kukicha ni kuzungumzia vibaya Manchester United na wachezaji wake.
✍🏿✍️Baada ya mchezo wa Jana kumalizika Kwa Uingereza Kupoteza dhidi ya timu ya taifa ya Iceland, walianza kumshushia lawama bwana mdogo kinda anaechipukia ambae ana muda mwingi zaidi wa kujifunza [ni Kobbie Mainoo] na kumuacha pacha wake aliecheza na Declan Rice, Wakati wote walitakiwa wawajibike.🥹🙄
✍🏿✍️Jambo la kushangaza zaidi hawakumjadili hata kidogo Declan Rice, ilibidi lawama nyingi ziende zaidi kwa Mainoo kuliko kwa Rice.🥺
✍🏿✍️Je, Kumlaumu Mainoo wakati Rice nae alikuwa na mchezo mbaya hiyo ni akili?🤷🏿♂️
✍🏿✍️Hii Hali imenirejesha nyuma kidogo ambapo Erik Ten Hag aliongea mara baada ya Fainali ya kombe la FA: 👇
Erik Ten Haag 🗣️"Nilikuwa na furaha sana kumtazama Kobbie Mainoo leo, lakini inabidi tuwe watulivu. Nyinyi hapa England ni wazuri sana katika kusifia wachezaji, na mameneja, Lakini munawatupia mzigo wa lawama pindi wanapopitia kipindi kigumu."
✍🏿✍️Vyombo vya habari vya uingereza, ni muda wa kujitathmini sasa, asilimia kubwa Ndivyo vinavyofukuzisha Makocha pale EPL.
DIC Sports 01 ✍🏿✍️ Naenda zangu..