Kassim Mgwami KD

Kassim Mgwami KD wasiliana nami KD kupitia WhatsApp 0755733099 au [email protected]

11/06/2026

World Cup 2026 hiyoooooooo, mambo ndio yameanza, lakini nawakumbusha makolo ligi inaendelea msijemkapigwa na Pamba, alafu mkasingizia World Cup 2026 haiwahusu. Kila timu ishinde mechi zake,msijizime data. Yanga daima mbele nyuma mwiko.

11/06/2026

Wananchi tunarudi kazini kwa sokwe wa Kigoma, kauli mbiu yetu ni ile ile kila timu ishinde mechi zake. Yanga daima mbele nyuma mwiko. Fisi Fc subirini wananchi waangushe kiganja mkiokote.

04/06/2026

Ukweli usemwe basi aina ya Irizar la makolo kwa msaada wa Jayrut ni chuma chakavu, afadhali basi la JKT Tanzania ni zuri kuliko hilo la makolo, maana la JKT Tanzania lilinunuliwa likiwa jipya kabisa kitu OG.

03/06/2026

Serengeti boys wanastahili heshima, lakini sio kuwafanya wabweteke kwani bado wana safari ndefu ya soka. Kinachotakiwa ni kuwa-boost wapate timu za kujiendeleza za Ulaya wakanoe vipaji vyao. Kwa upande wa TFF hilo ni somo wanatakiwa waheshimu soka la vijana, walisimamie vizuri zaidi ya hapa, waache masuala ya zimamoto k**a walivyozoea.

02/06/2026

Timu pekee itakayoleta 🏆 ya Afrika hapa Tanzania kwa mara ya kwanza ni Yanga.

02/06/2026

Tujikumbushe: Fainali za kombe la Dunia mwaka 1990 Cameroon waliwafunga Colombia 2-1,magoli yote yalifungwa na Roger Miller.

01/06/2026

Makolo kucheza mchana kwenye jua la utosi sio mara ya kwanza walishawahi kwenye ligi hii hii kucheza na Tanzania Prisons saa saba mchana kwenye shamba la bibi kwa maelekezo ya DSTV ili mechi hiyo irushwe mubashara na Supersport 3.

01/06/2026

Tujikumbushe:Kombe la dunia la mwaka 1990 Cameroon iliwafunga mabingwa watetezi Argentina 1-0 uku Cameroon wakiwa na wachezaji wawili pungufu,baada ya wachezaji Kana Biyk na Benjamin Massing kupigwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo.

31/05/2026

Makolo msijisahaulishe ligi bado haijaisha,kwa wananchi ndio kwanza imeanza. Yanga daima mbele nyuma mwiko. Kila timu ishinde mechi zake.

30/05/2026

Yanga hakuna kulala, mikakati yetu iko palepale,na kauli mbiu yetu ya "kila timu ishinde mechi zake" iko palepale tusijisahau kipindi hiki cha FIFA break,makolo wataitumia hiyo nafasi kutuhujumu. Yanga daima mbele nyuma mwiko.

Address

Kidatu, Kilombero
Morogoro

Telephone

+255755733099

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kassim Mgwami KD posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kassim Mgwami KD:

Share