01/09/2026
Mchambuzi wa michezo wa Wasafi FM, Ricardo Momo, amesema mshambuliaji wa Simba SC, Libasse Gueye, anastahili zaidi kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti. Momo amesema Gueye amekuwa na kiwango kizuri katika michezo yake ya mwanzo ya msimu, akionyesha mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba.
Hata hivyo, Momo amekiri kuwa Maxi Nzengeli naye anastahili kupewa nafasi katika mjadala huo kutokana na kiwango kizuri alichoonyesha katika michezo mitano aliyocheza. Pamoja na wote kuwa na kiwango kizuri, Momo anaona Gueye anastahili zaidi tuzo hiyo kutokana na mchango wake kwenye timu. Ricardo Momo amemuweka Gueye mbele ya Maxi Nzengeli katika mbio za Mchezaji Bora wa Agosti.