02/11/2021
JICHO MAKINI KWENYE 90 ZA YAรGA SC NA RUVU SHOOTING.
Leo ilikuwa ni Mayele Vs Mohammed Makaka. Mashuti manne(4) ya Mayele yaliyo lenga lango yaliokolewa na Makaka Kwa ustadi mkubwa. Makaka ni miongoni mwa Magoli Kipa wazuri na wenye ubora sana kwenye hesabu.
Timu ilimmiss Khalid Aucho.Muunganiko na ushirikiano wa Yannick Bangala na Mukoko haukuwa kwenye Kiwango bora k**a ule wa Aucho na Mukoko. Aucho mara hucheza karibu sana kwenye pivot, Mukoko alicha nafasi kubwa kati yake na Bangala.
Djuma Shabani hakuwa na ufanisi Mkubwa leo hasa kabla ya kadi nyekundu ya Santos, Alipoteza pasi kadhaa. Niliamini baada ya Yanga kuongoza basi mabadiliko ya kumuingiza David Bryson yangekuwa kwa Djuma ili Kibwana aende kulia. Djuma anaonekana alitumia nishati kubwa kwenye Derby dhidi ya Azam FC.
Mkwasa alikuwa na mipango bora sana hasa kwenye alipo amua Kucheza kwenye falsafa ile ile ya umiliki wa mpira. Walifanikiwa kwa asilimia kadhaa walifanya play out from the back,walifanikiwa na build-up yao ilifia Katikati ya Uwanja. walikosa njia bora ama link-up Man kwenye kiungo na ushambuliaji.
Kadi nyekundu ya Santos Mazengo Ilibadili muelekeo kiuchezaji na mipango kiujumla (game approach) Kwa Ruvu Shooting. Baada ya kucheza kwenye total football na kurudi kufanya Low block huku wakitumia Counter Attack. Iliwarejesha Sana Yanga kwenye wepesi wa kuumiliki mchezo.
Emmanuel Mwandembwa ni miongoni mwa Waamuzi bora Nchi. Kadi nyekundu ilikuwa sahihi Kwa asilimia ๐ฏ na, pigo la huru la penati lina maswali mengi sana hasa kwenye kuligundua k**a sio ama ndiyo. Ila Kwa namna ilivyo tokea basi Mwamuzi yeyote anaweza kutoa ama kutokutoa pia. Tukio tata.