Global Foot

Global Foot Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Global Foot, Sports Event, Osofia, Kigoma.
(1)

Msafiri Sports Hub | Taarifa Moto za Michezo
⚽️ Habari, Matokeo & Takwimu
🌍 EPL | La Liga | Serie A | Bundesliga | Ligue 1 | NBC
🔥 Hashtags
📲 Matukio Mubashara & Uchambuzi

KWA MATANGAZO KARIBU
PIGA 0756170880

🚨 KOMBE LA DUNIA 2026 LINAANZA LEO, LAKINI KUNA MAMBO YANAYOIBUA MASWALI MAKUBWA! 🌍⚽Wakati dunia ikisubiri kwa hamu mech...
11/06/2026

🚨 KOMBE LA DUNIA 2026 LINAANZA LEO, LAKINI KUNA MAMBO YANAYOIBUA MASWALI MAKUBWA! 🌍⚽

Wakati dunia ikisubiri kwa hamu mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia 2026, matukio kadhaa ya kushangaza na yenye utata yameripotiwa siku chache zilizopita:

🇨🇭 Mshambuliaji wa Uswisi, Embolo, alichelewa kujiunga na timu kutokana na matatizo ya visa.

🇮🇶 Nyota wa Iraq, Aymen Hussein, alihojiwa kwa karibu saa 7 baada ya kuwasili nchini Marekani.

🇮🇷 Iran ilikumbwa na changamoto kubwa za visa, huku wajumbe wao 15 wakinyimwa vibali vya kuingia.

🇸🇴 Omar Artan wa Somalia, aliyeshinda tuzo ya Mwamuzi Bora wa Afrika 2025 kutoka CAF, alinyimwa ruhusa kuingia Marekani na hivyo kuukosa mashindano hayo.

🇿🇦 Wajumbe wa Afrika Kusini uliwasili kwa kuchelewa baada ya baadhi ya wanachama kushindwa kupata visa kwa wakati.

🇸🇳 Baadhi ya maafisa wa Senegal walifanyiwa ukaguzi mkali wa usalama, wakalazimishwa kuvua viatu, jambo lililosababisha madai ya ubaguzi.

🇺🇿 Timu ya Uzbekistan ilikaguliwa kwa kutumia mbwa wa kunusa mabomu, huku video za tukio hilo zikisambaa duniani kote.

🏴󠁧󠁢󠁳󠁣󠁴󠁿 Baadhi ya mashabiki wa Scotland walifutiwa vibali vya ESTA siku chache kabla ya safari zao.

💸 Mashabiki wengi waliokuwa tayari wamenunua tiketi na kuweka nafasi za hoteli walikataliwa visa, na hivyo kupoteza fedha nyingi sana.

👇 Wewe unaonaje?
Kombe la Dunia linapaswa kuunganisha watu wote bila vikwazo, au usalama wa nchi mwenyeji unapaswa kupewa kipaumbele hata k**a wengine wataathirika?

🔥 Je, haya ni matukio ya kawaida au kuna jambo kubwa zaidi linaendelea nyuma ya pazia? 👇⚽🌍

Kuna nini kinaendelea hapa...
26/05/2026

Kuna nini kinaendelea hapa...

Real Madrid walimwacha Samuel Eto’o akiwa na miaka 16 peke yake kabisa kwenye uwanja wa ndege wa Barajas, Madrid.Hakukuw...
25/05/2026

Real Madrid walimwacha Samuel Eto’o akiwa na miaka 16 peke yake kabisa kwenye uwanja wa ndege wa Barajas, Madrid.
Hakukuwa na kiongozi wa klabu wa kumpokea.
Hakukuwa na mtafsiri.
Hakukuwa hata na gari la kumchukua.

Alikuwa ni kijana mdogo kutoka Cameroon, mwenye ndoto ya soka na hakuwa hata anajua aende wapi.
Mtu mmoja aliyekuwa anafanya kazi ya usafi usiku barabarani — Mwafrika mwenzake — alimwona akiwa amepotea, akamsubiri na kumpeleka mwenyewe hadi kwenye uwanja wa mazoezi wa Real Madrid. Mpaka leo Eto’o bado ana mawasiliano na huyo mtu.

Na hicho ndicho kilikuwa “ukaribisho” wake Madrid.
Badala ya kupewa nafasi, Real Madrid wakamzungusha kwa mikopo Leganés, Espanyol na Mallorca. Hakuna imani. Hakuna nafasi ya kweli ya kuonyesha uwezo wake.

Mwaka 2000, baada ya tayari kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki na AFCON akiwa bado mdogo, Madrid wakamuuza kwa pauni milioni 4.4 tu.

Akiwa Mallorca ndipo dunia ilianza kumuona Samuel Eto’o halisi.
Magoli 70.
Mfungaji bora wa klabu.
Mchezaji Bora wa Afrika mara mbili.
Florentino Pérez alipojaribu kumrudisha Madrid… Alikuwa tayari amechelewa.

Barcelona wakamnunua kwa euro milioni 24 — karibu mara tano ya fedha ambazo Madrid walimuuza.
Na Eto’o hakusahau alivyopuuzwa.

Mwaka 2005 Barcelona walipotwaa La Liga, Eto’o alisimama Camp Nou mbele ya mashabiki 98,000 na kuongoza nyimbo za kubeza Madrid:
“Madrid bastards, salute the champions!”
Alipigwa faini ya euro 12,000.
Lakini kwake haikuwa pesa — ilikuwa ni kisasi cha heshima yake.

Baadaye akaenda kufunga kwenye fainali tatu tofauti za UEFA Champions League na kuweka historia kwa kushinda trebles mbili mfululizo akiwa na klabu mbili tofauti — jambo ambalo hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kufanya.

Yote haya… yalianza siku ambayo Real Madrid walishindwa hata kutuma gari la kumfuata kijana mmoja kutoka Cameroon.

Na hapo ndipo Historia ya mpira ilibadilika milele. 👀🔥

Wakala wa FIFA kutoka nchini Uganda, Ronnie Santos Mwine Fred ameripoti kuwa, Maskauti wa vigogo wa 🇹🇷Uturuki Fenerbahçe...
12/05/2026

Wakala wa FIFA kutoka nchini Uganda, Ronnie Santos Mwine Fred ameripoti kuwa, Maskauti wa vigogo wa 🇹🇷Uturuki Fenerbahçe SK wamekuwa 🇹🇿Tanzania kwa siku ya 4 sasa, na sababu pekee ni nyota kijana wa timu ya taifa ya 🇺🇬Uganda "The Cranes" Allan Okello!
Na Watamfuatilia tena katika mchezo ujao dhidi ya Dodoma Jiji.

Katika mechi ya kwanza waliyomtazama, alifunga mabao 2 na kutoa assist 1 dhidi ya Coastal Union

Young Africans S.C. wanatajwa kuhitaji takribani dola milioni 3 (Tsh 7.8B) kwa nyota huyo wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.

Mwaka 2005, Peter Crouch alipojiunga Liverpool, alitumia wiki yake ya kwanza akiishi hotelini ambapo alimpenda kimyakimy...
09/05/2026

Mwaka 2005, Peter Crouch alipojiunga Liverpool, alitumia wiki yake ya kwanza akiishi hotelini ambapo alimpenda kimyakimya mmoja wa wahudumu wa mapokezi (receptionist).

Akiwa mazoezini, hakuweza kujizuia kumzungumzia mwanamke huyo kwa wachezaji wenzake wapya, akieleza jinsi alivyokuwa mrembo na jinsi alivyofikiri ana nafasi ya kumpata.

Hapo ndipo Jamie Carragher alipowaita wachezaji wote na kumwambia Crouch arudie alichokuwa akisema.
Kwa kujiamini, Crouch aliendelea kumsifia, akidiriki hata kukiri kuwa alikuwa akimfikiria mwanamke huyo kutwa nzima.

Kisha likaja tukio lililopindua kila kitu.
Mhudumu huyo wa mapokezi… kumbe alikuwa ni mke wa mchezaji mwenzake mpya, Xabi Alonso. 🤣

Wachezaji wote waliangua kicheko baada ya kubaini hilo...

Ulianza kuangalia Kombe la Dunia mwaka gani?
01/05/2026

Ulianza kuangalia Kombe la Dunia mwaka gani?

🚨 RASMI: Burnley wametangaza kocha kuwa Scott Parker ameondoka katika klabu hiyo.Michael Jackson atakuwa kocha wa muda h...
01/05/2026

🚨 RASMI: Burnley wametangaza kocha kuwa Scott Parker ameondoka katika klabu hiyo.

Michael Jackson atakuwa kocha wa muda hadi mwisho wa msimu.

fungua comment kuona picha nyingine ya kocha Michael Jackson.

Mykhailo Mudryk amefungiwa miaka 4 na FA baada ya kushindwa kesi ya dawa za kulevya ya mwaka 2024. Nyota huyo wa Chelsea...
30/04/2026

Mykhailo Mudryk amefungiwa miaka 4 na FA baada ya kushindwa kesi ya dawa za kulevya ya mwaka 2024. Nyota huyo wa Chelsea F.C. anatarajiwa kukata rufaa katika mahak**a ya usuluhishi wa michezo (CAS) .

Hebu angalia hii story kwa jicho la biashara ya mpira:
🔸 Alisajiliwa kwa €100M 💰
🔸 Akapewa mkataba wa miaka 7 (£100,000 kwa wiki)
🔸 Hajacheza kwa takribani miaka 2 😳
🔸 Sasa amefungiwa miaka 4 🚫
🔸 Na bado atabakiwa na mwaka 1 kwenye mkataba wake baada ya kifungo kuisha

Hii siyo tu hasara… ni project iliyofeli kabisa.

Je, huu ndiyo usajili mbaya zaidi kuwahi kutokea kwenye Premier League? 📉 🤔

Anaitwa Mimisa Masato kutoka Kenya... Ndiye alikuwa mwamuzi wa fainali ya Kombe la Muungano kati ya Simba SC vs Yanga SC...
30/04/2026

Anaitwa Mimisa Masato kutoka Kenya...
Ndiye alikuwa mwamuzi wa fainali ya Kombe la Muungano kati ya Simba SC vs Yanga SC.

Kwa ulivyomuona unampa asilimia ngapi?
Ana utofauti gani na Marefa wa Tanzania?

MWENYE KITI WA BODI YA LIGI YA NBC ANAWEZA KUSEMA HIVI? 🚨🗣️ JAVIER TEBAS [Rais wa La Liga]:“Barcelona inaweza kufikisha ...
30/04/2026

MWENYE KITI WA BODI YA LIGI YA NBC ANAWEZA KUSEMA HIVI?

🚨🗣️ JAVIER TEBAS [Rais wa La Liga]:

“Barcelona inaweza kufikisha pointi 100 kwenye ligi? SIPENDI timu kufikisha pointi 100, ni nyingi sana.

Ni kweli kwamba Real Madrid na Atlético Madrid zimepoteza pointi nyingi na ziko chini ya kiwango chao cha kawaida, lakini sipendi bingwa kufika zaidi ya pointi 90.”

“Napenda ligi ambazo zinapata bingwa siku ya mwisho wa msimu.
Ndiyo maana ningependelea Barça isichukue ubingwa kwenye El Clásico.” 😂🤡

“Natumaini FC Barcelona hawatashinda ligi kwenye El Clásico wala kufikisha pointi 100.”

Sasa fikiria hali k**a hii ingetokea kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara… Mwenyekiti wa bodi ya ligi anasema wazi hataki bingwa awe na pointi nyingi au ashinde mapema 😅

Hapo ndipo ungeona presha ya mashabiki wa Young Africans, S.C., Simba S.C. na wengine ikipanda juu sana—wengine wakisema ligi inapangiwa matokeo, wengine wakisema ushindani unapotezwa makusudi.

Kwa kifupi, kauli k**a hizi zinaweza kuongeza drama na mjadala mkubwa kuliko hata matokeo yenyewe... 🔥

Address

Osofia
Kigoma
ELKAKA

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Global Foot posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Global Foot:

Share

Category