11/07/2026
Nyota wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini na klabu ya Mamelodi Sundowns, Jayden Adams amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 25, ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kuiwakilisha Bafana Bafana kwenye michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026.
Adams alicheza mechi zote za Afrika Kusini kwenye michuano hiyo isipokuwa mchezo wa hatua ya 32 bora kwenye kipigo cha 1-0 dhidi ya Canada huku vyanzo mbalimbali vikieleza kuwa alijiua nyumbani kwake huko Stellenbosch hatua inakuja baada kuomboleza kifo cha bibi yake mwenye umri wa miaka 72, Marianna Adams wakati akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa huko Marekani.
Adams, pamoja na wachezaji wengine saba wa Mamelodi Sundowns walioiwakilisha Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia, walipewa likizo ya wiki mbili zaidi kabla ya kurejea kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya na alitarajiwa kujiunga tena na kikosi cha klabu hiyo wiki ijayo kwa ajili ya kambi ya mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya huko Austria.
Kiungo huyo ambaye ni zao la akademi ya Stellenbosch alikuwa sehemu ya kikosi cha Bafana Bafana kilichoshinda medali ya shaba kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2024) huko Ivory Coast, kifo chake kimesababisha mshtuko mkubwa katika soka la Afrika Kusini.
fans