16/11/2019
Deo Kanda yule mtu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yule fundi mmoja kutoka viunga kwa Kamarondo pale Lubumbashi
Deo kaja Tanzania kuchukua nafasi ya Prince wa Msimbazi, kipenzi cha wanasimba Immanuel Okwi, tafsiri ya haraka na ukubwa wa jina lake ni wazi tulifahamu viatu vitamtosha haraka
Kocha wake Lamine N'diaye alimuhusudu sana, ile TP iliyojaa mafundi wa kila rangi mtu wangu, ila Deo alicheza, ujio wake hapa Bongo sikutarajia makubwa, naona k**a upepo umekata sana
Sio lazima sana Mzamiru acheze k**a Mbenza Bedi yule, sio lazima Shiboub acheze k**a Dioko Kaluyituka yule, sio lazima pacha wake awe Ngandu Kasongo yule au Given Singuluma, ni wazi ameshuka sana Deo
Kuna vitu vya kiufundi labda vinamtatiza, Deo pale Lubumbashi walimtumia mara nyingi k**a Forward na k**a anacheza pembeni ni k**a wide forward, ila kwa Simba naona kuna Meddie eneo hilo, lazima operation ya Deo iwe chini
Mbaya zaidi kucheza pembeni kasi yake haiendani na Mohamed Hussein, MO anataka upepo wa winga muda wote, Deo alienjoy TP alipokuwa na Kiritsho Kasusula, walielewana sana kwakua pumzi zilikuwa leveled, ila sasa kuna disparity kubwa sana kati yake na leftback wake
Kwa hype aliyonayo sasa naona atastruggle ndani ya Simba, mfumo unahitaji pumzi, vision na utulivu, Deo ana skills sana, ila kuna wakati modern football inataka unyumbufu wa kimfumo, kuna wakati unamwona mwili unataka ila akili haitaki
Huenda ikawa ramli chonganishi 😁😂ila frankly speaking Deo hakupaswa kuja sasa kwenye Simba hii na aina yake ya game, k**a Deo angekuwa beki nisingekataa ila kwenye eneo lake linataka extra potentials, which yeye kwasasa muda umeenda sana
Miraji Athuman, Hassan Dilunga na Rashid Juma wanaweza kufanya anachofanya na zaidi, so bad for him, so bad for him, Deo cool down yoh, time is up