10/12/2021
TIMU NDOGO ZIJIFUNZE "UASI"
Simba anapata pesa toka sportpesa, Azamtv matangazo, Azamtv maudhui ya picha, emirates, ATCL, kampuni ya mabasi ya Azim dewji, Mo Dewji na kampuni zake za Metl nk
Simba ameuza wachezaji Miquisone na chama kwa zaidi ya bilioni 3, hao ni wachezaji wawili tu..
Simba anapata pesa nyingi toka kwenye viingilio vya uwanjani, pesa za mashindano kimataifa, michango ya wanachama nk..inshort simba na Yanga kwenye maisha ya kawaida ni matajiri..
Hebu tufikirie timu nyingine ndogo k**a Mbeya Kwanza, Mbeya City, Geita Gold, Biashara Mara, Dodoma Jiji, Coastal union, Prisons nk, vipato vyako kwa mwaka vipoje? Wakati kipato cha Simba kwa kumuuza mchezaji mmoja inazungumzia bilioni hivi mbeya City inaweza kuuza mchezaji angalau kwa mil 100? Hivi wanaweza kufikisha walau Bilioni 1 katika viiingilio vyao mlangoni kwa msimu mzima? Nini hasa source ya kipato chao!?
Nataka kusema timu ndogo zijifunze uasi, ni lazima watafute umoja wao dhidi ya hizi klabu kubwa mbili za kkoo, Simba na Yanga hawaogopi kuasi timu nyingine kwa kukataa udhamini kwa sababu wamekula wameshiba, hawajui k**a wenzao wana njaa, k**a timu ndogo hazitaungana kutetea maslahi yao na kuacha simba na Yanga wateke mijadala na kupanga masharti dhidi ya wawekezaji basi hapo wa kuumia sio TFF ni wao, UASI sio dhambi unapofanywa kwa nia njema, nashauri timu ndogo "ZIASI" wakubwa hawa wawili kwa faida yao