11/06/2026
Mchezaji wa Timu ya taifa ya Mexico Julian Quinones ameweka rekodi ya kufunga bao la kwanza la ufunguzi kombe la Dunia mwaka 2026 katika mchezo dhidi ya Afrika Kusini.
Quinones amefunga bao hilo leo Juni 11, 2026 kwenye mechi ya ufunguzi dhidi timu ya taifa ya Afrika Kusini mchezo uliopigwa katika dimba la Mexico city Nchini Mexico.
Ikumbukwe katika mashindano ya kombe la Dunia kwa mwaka 2010 Afrika Kusini ilicheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Mexico, mchezo uliotamatika kwa sare ya 1-1 kwa upande wa mfungaji wa goli la kwanza katika michuano hiyo alikuwa ni Siphiwe Tshabalala kutoka Afrika Kusini huku bao la kusawazisha likifungwa na Rafael Márquez.