20/07/2017
BRAINPOWER CONSULTANCY
UCHAMBUZI WA KUFAHAMU HAIBA -TABIA, UWEZO KITAALUMA, NJIA RAFIKI YA KUJIFUNZA, VIPAJI NA KARAMA ZA MTOTO
Kila binadamu amejaliwa na Muumba wake (MUNGU) uwezo fulani wa kitaaluma, vipaji, na karama ili aweze kuutumia hapa duniani k**a nyenzo katika kuufikia ufalme wa muumba wake.
Hata hivyo, mara nyingi wazazi wengi hushindwa au huchukua muda mrefu wa kubaini uwezo asilia wa mtoto katika eneo fulani. Hali hii hupelekea mtoto au mtu mzima kutotumia kabisa au kuchelewa sana kubaini na kutumia kipaji chake kiasi cha kushindwa kujiletea maendeleo binafsi, ya familia na taifa kwa ujumla. Kimsingi kila binadamu ni mtu maarufu sana ikiwa tu atawezeshwa na kusaidiwa kubaini uwezo wake asilia katika eneo husika ili aweze kuitiisha au kuistaajabisha hii dunia.Mila, tamaduni, desturi , uchumi, siasa, vyombo vya habari(media), kundi rika (peers) na marafiki ni moja ya sababu zinazokwamisha watu kutojua na kutotumia vipaji na uwezo wao asilia. Uwezo wa mtoto huishia kuachwa na kupuzwa na hivyo kufanya mzunguko wa umaskini wa kutupwa (vicious cycle of poverty) kuendelea kushamiri katika kaya, jamii na taifa kwa ujumla.
Inaendelea ukurasa unaofuata
Watoto ni rasiliamali pekee ya familia na taifa kwa ujumla kwani hatima ya taifa letu ipo mikononi mwa watoto wetu. Mzazi yeyote anayeshindwa kuwekeza(Elimu na Nidhamu) kwa mtoto katika eneo lake asilia anatengeneza jamii dhaifu na taifa dhaifu.
Je wajua kuwa fursa ya mafanikio ya mtoto wako inapatikana kwenye haiba yake? Kila mtoto ana karama na vipaji ambavyo vikigundulika mapema vyaweza kuwa ni chachu kubwa ya maendeleo yake binafsi na kwa taifa lake.”Hayupo mtoto duniani ambaye ni “kilaza” yaani mjinga. Kila mtoto anaakili hasa akiwa katika eneo lake analolimudu zaidi kutokana na uasili wake. Huwezi ukamhukumu samaki kwa kushindwa kupanda juu ya mti kwa kuwa sio eneo lake asilia. Vivyo hivyo huwezi kumhukumu nyani kwa kushindwa kuogelea ndani ya bwawa la maji kwa kuwa sio eneo lake asilia.
Hivyo basi hekima ya mzazi na serikali kwa ujumla ni kuwekeza kwa mtoto hasa baada ya kubaini haiba, vipaji na karama za mtoto. Kupitia huduma hii, uchambuzi wa kina wa haiba, na ugunduzi wa vipaji na karama za mtoto utafanyika na mwisho ushauri na ripoti ya kina itatolewa.
BPC inaweza kwa asilimia 85 hadi 95 kubaini haiba- tabia, uwezo wa kitaaluma, njia rafiki ya kujifunza, karama na vipaji vya mtoto kupitia sayansi ya alama za vidole –Dermatoglyphics (the scientific study of fingerprints) na sayansi ya maumbile na kazi za sehemu mbalimbali za ubongo wa binadamu-neuroscience (scientific study of human brain) pamoja na elimu ya tabia za binadamu (psychology), vile vile kupitia tafiti maarufu iliyofanywa na Daktari Howard Gardner ( The eight multiple intelligence) na Carl Jung (the sixteen personalities).
Kuishi na mtoto pasipo kufahamu uwezo wake kitaaluma, karama na vipaji vyake ni sawa na kuchezea kipande cha jiwe pasipokujua kuwa hicho kipande ni dhahabu yenye thamani kubwa inayoweza kubadili hali ya maisha ya familia yako na taifa kwa ujumla.
Karibu sana
Tunapatikana hapa hapa Iringa Mjini kata ya Mivinjeni , katikati ya Msikiti wa Hidaya na Hoteli ya Longoi.
GERVAS BATISTER MGAYA
BPC DIRECTOR
Barua pepe: [email protected],Nambari ya simu :+255768683758, Iringa Mjini
Siri ya Mafanikio ni Kujitambua mwenyewe na kuitumia hiyo fursa kwa nguvu zako zote