01/05/2023
JINSI YA KUMALIZA VIZURI
Na Mch: Chambo
Andiko: 2 Timotheo 4: 6-7
2 Timotheo 4:5-8
Dhima kuu: Maagizo ya mwisho ili kumtia moyo Timotheo katika huduma. Paulo alitamani kuona kijana wake Timotheo amalize vizuri
[6]Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
[7]Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;
(8)sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana,mwamizi wa haki, atanitunukia siku ile: wala SI Mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kw shauku kudhihirishwa kwake.
# Mifano ya wa watu walioanza vizuri na wak**aliza vibaya
1. Sauli alianza vizuri na Mungu lakini ak**aliza vibaya, mwanzoni alikubali kuongozwa na Mungu badae anaongozwa na mwanamke Mwenye Pepo la uaguzi na kuanzia hapo akapoteza ushirika na Mungu
2. Yuda Iskarioti alianza vizuri na Yesu lakini badae ak**aliza vibaya Kwa kumsaliti Yesu
3. Dema alianza vizuri na Mungu lakini mwishoni anapenda ulimwengu Kwa kuiacha Imani.
MAMBO MATATU YA KUJIFUNZA JINSI NA NAMNA YA KUMALIZA VIZURI
1. Pigana vita vizuri vya Imani, mkristo anatakiwa KUTAMBUA kuwa Yuko katika vita, biblia inasema vaeni silaha zote za Mungu, inatakiwa kuwa mpambanaji
Waefeso 6:10-11
[10]Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
[11]Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
2 Wakorintho 10:3-5
[3]Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;
[4](maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
[5]tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
A. MAOMBI NI SILAHA INAYOSAIDIA KUMALIZA VIZURI
B. NENO NI SILAHA INAYOSAIDIA KUMALIZA VIZURI
C. KUMTUMIKIA MUNGU KWA UAMINIFU NI SALAHA NZURI YA KUSHINDA VITA.
2. Mwendo , kaza mwendo
Waebrania 12:1-2
[1]Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
[2]tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
DHAMIRIA KWENDA MBINGUNI
3. Linda Imani Yako -ukitaka kumaliza vizuri Linda Imani Yako sana