SokaOnline

SokaOnline Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from SokaOnline, Sports, Dar es Salaam.
(2)

🚨 Kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya Argentina, Enzo Fernández, amezua mjadala mtandaoni baada ya kauli yake kuhusu h...
02/09/2026

🚨 Kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya Argentina, Enzo Fernández, amezua mjadala mtandaoni baada ya kauli yake kuhusu hamu aliyokuwa nayo ya kucheza katika klabu ya Manchester City.

Enzo amefunguka kuwa tangu akiwa kijana alikuwa na ndoto ya kuchezea klabu kubwa k**a Manchester City, akivutiwa na mfumo wa uchezaji pamoja na mafanikio ya timu hiyo chini ya Pep Guardiola.

"Licha ya kuipenda sana klabu hii, ukweli ni kwamba tangu nikiwa mdogo nilikuwa na ndoto ya kucheza kwenye klabu kubwa k**a Manchester City. Ni timu inayovutia sana kwa jinsi inavyocheza na mafanikio iliyonayo." — Kauli ya Enzo Fernández

Kauli hii imepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa Chelsea, ikizingatiwa kuwa alijiunga na Blues kwa ada ya rekodi ya pauni milioni 106.8 mapema mwaka 2023 akitokea Benfica.

🚨 Jamie Carragher amemtaja Riccardo Calafiori k**a beki wa kushoto bora zaidi katika Premier League kwasasa. Carragher a...
02/09/2026

🚨 Jamie Carragher amemtaja Riccardo Calafiori k**a beki wa kushoto bora zaidi katika Premier League kwasasa.

Carragher amesifu muundo imara wa ulinzi unaowekwa na Mikel Arteta, ambao unawapa mabeki wa pembeni uhuru wa kushambulia na kubadilishana nafasi uwanjani.

Pamoja na ushawishi wa Calafiori, Carragher ameitaja Arsenal k**a timu bora zaidi ulimwenguni kwa sasa kutokana na uwezo wao wa kutawala na kushinda mechi ngumu za ugenini.

Calafiori akiwa na Arsenal msimu huu hadi sasa

⚽️ vs Manchester City (🏆)
🅰️ vs Coventry City
🅰️ vs Aston Villa

🚨 Taarifa iliyotolewa na gazeti la Le Parisien nchini Ufaransa imefichua kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa na ms...
02/09/2026

🚨 Taarifa iliyotolewa na gazeti la Le Parisien nchini Ufaransa imefichua kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa na mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappé, alikuwa miongoni mwa watu waliolengwa kwenye mtandao wa utekaji na uvamizi wa majumbani (home invasion).

Jeshi la Polisi na waendesha mash*taka nchini Ufaransa wamemk**ata kijana mmoja mwenye umri wa miaka 18 ambaye anatuhumiwa kuratibu mpango huo uliolenga zaidi ya watu 26, wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wanamuziki.

Kijana huyo amewekwa kizuizini huku akikabiliwa na mashtaka mazito ya kupanga matendo ya utekaji na uvamizi wa kigaidi/kiharifu.

Mamlaka nchini Ufaransa zinaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini iwapo kijana huyo alikuwa akifanya kazi na mtandao mpana zaidi wa kiharifu.

🚨 Aliyekuwa Mshambuliaji wa Fc Barcelona, Robert Lewandowski, ametoa mtazamo wake kuhusu mabadiliko na ushindani wa La L...
02/09/2026

🚨 Aliyekuwa Mshambuliaji wa Fc Barcelona, Robert Lewandowski, ametoa mtazamo wake kuhusu mabadiliko na ushindani wa La Liga 🇪🇸 msimu huu katika mahojiano yake na jarida la Diario AS.

Lewandowski amekiri kuwa wapinzani wao wakubwa, Real Madrid, wamekuwa imara zaidi ukilinganisha na msimu uliopita kutokana na ujio wa kocha José Mourinho pamoja na usajili wa wachezaji wapya, lakini akasisitiza kuwa imani yake bado ipo kwa Barcelona.

🗣️ Kauli ya Robert Lewandowski:

"Real Madrid ni timu nzuri na imara zaidi wakiwa na José Mourinho pamoja na usajili wao mpya. Baada ya miaka miwili bila kutwaa mataji, saikolojia na mtazamo wao (mentality) ni vitu vya msingi sana na wanaweza kuwa na nguvu kubwa msimu huu, lakini mimi siku zote nasimama na Barcelona, naamini Barcelona itakuwa bora zaidi."

🚨 Mshambuliaji, Julian Alvarez 🇦🇷 amekataa ofa ya kujiunga na Arsenal 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 na kuamua kuendelea kuitumikia Atlético Ma...
01/09/2026

🚨 Mshambuliaji, Julian Alvarez 🇦🇷 amekataa ofa ya kujiunga na Arsenal 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 na kuamua kuendelea kuitumikia Atlético Madrid 🇪🇸

Licha ya jitihada zilizofanyika pande zote mbili za Arsenal na Atlético, Julian aliendelea kusisitiza kuwa ndoto yake ni kuhamia Fc Barcelona na sio timu nyingine yoyote.

Alvarez amekubali kubaki baada ya Atlético kukataa kumuuza kwenda Barcelona na bado anaamini kuwa ndoto yake itatimia katika madirisha yajayo.

🚨 Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uhispania, Luis de la Fuente, amemwagia sifa kedekede kiungo mpya wa FC Barcelona, Rodr...
01/09/2026

🚨 Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uhispania, Luis de la Fuente, amemwagia sifa kedekede kiungo mpya wa FC Barcelona, Rodri.

Akimulika usajili wa Rodri kutoka Manchester City kwenda Barcelona, De la Fuente aliiambia Radio Marca kuwa uwezo wa kiungo huyo unamfanya aweze kuingia na kufanya vizuri katika mfumo wowote au timu yoyote duniani bila shida.

🗣️Kauli ya Luis de la Fuente:

"Itakuwa rahisi kwake kuzoea, kwa sababu Rodri ni Messi wa soka la Uhispania. Kwa hiyo ataingia na kufanya vizuri katika timu yoyote na chini ya mazingira yoyote. Yeye ndiye mchezaji bora zaidi duniani katika nafasi anayocheza.

Ninachofurahia ni kuona wachezaji hawa wakubwa wakirejea kwenye klabu za La Liga, kwa sababu inafanya ligi yetu kuwa kubwa zaidi na kuwafanya wachezaji bora duniani kushindana hapa nyumbani.

Ningefurahi sana kuona wachezaji wengi zaidi waliopo nje wanarejea na kuonyesha vipaji na viwango vyao vikubwa ndani ya vilabu vya hapa nyumbani"

🚨 Meya wa Wilaya ya Yomra katika mji wa Trabzon, Mustafa Bıyık, amewasilisha pendekezo rasmi katika Baraza la Manispaa k...
01/09/2026

🚨 Meya wa Wilaya ya Yomra katika mji wa Trabzon, Mustafa Bıyık, amewasilisha pendekezo rasmi katika Baraza la Manispaa kubadilisha jina la mtaa anaokwenda kuishi nyota mpya wa Trabzonspor, Mohamed Salah, ili kumpa heshima ya kipekee.

Mtaa huo uliokuwa ukiitwa Selvi Street na sasa utajulikana rasmi k**a "Mohamed Salah Street"

🗣️ Kauli ya Meya Mustafa Bıyık (kupitia X):

"Tuna furaha kubwa sana, Mohamed Salah ni usajili mkubwa zaidi sio tu katika historia ya Trabzonspor, bali katika historia ya soka la Uturuki, anaenda kuishi katika wilaya yetu.

Uwepo wa staa wa kiwango hiki duniani hapa Yomra kutaongeza thamani kubwa ya kibiashara na kuitangaza wilaya yetu. Ndio maana wiki hii kupitia uamuzi wa baraza tutabadilisha jina la mtaa anaoishi kuwa 'Mohamed Salah Street'. Sisi tumetimiza wajibu wetu, sasa ni zamu ya Salah kutimiza majukumu yake uwanjani"

Raphinha na Kylian Mbappe wameanza kuwaka mapema sana katika mechi tatu za La Liga zilizochezwa hadi sasa:Raphinha 🇧🇷 - ...
01/09/2026

Raphinha na Kylian Mbappe wameanza kuwaka mapema sana katika mechi tatu za La Liga zilizochezwa hadi sasa:

Raphinha 🇧🇷 - Barcelona
🏟️ Mechi: 3️⃣
⚽ Mabao: 5️⃣
🅰️ Assist: 1️⃣

Kylian Mbappe 🇫🇷 - Real Madrid
🏟️ Mechi: 3️⃣
⚽ Mabao: 4️⃣
🅰️ Assist: 0️⃣

Nani atamaliza akiwa na mabao mengi?

FULL TIME ⏰Barcelona 5️⃣ ➖ 2️⃣ Rayo Vallecano⚽ 12' Camello (🅰️ García)⚽️ 19' Raphinha (🅰️ Xavi Espart)⚽️ 21' Lamine Yama...
31/08/2026

FULL TIME ⏰

Barcelona 5️⃣ ➖ 2️⃣ Rayo Vallecano

⚽ 12' Camello (🅰️ García)
⚽️ 19' Raphinha (🅰️ Xavi Espart)
⚽️ 21' Lamine Yamal (🅰️ Bernal)
⚽️ 51' Lejeune (OG)
⚽️ 59' Camello (🅰️ Lopez)
⚽️ 71' Raphinha (🅰️ Gordon)
⚽️ 90' Lamine Yamal (🅰️ Adeyemi)

MSIMAMO

1. Barcelona - Pts 9️⃣ (Mechi 3)
2. Real Madrid - Pts 9️⃣ (Mechi 3)
3. Atlético - Pts 7️⃣ (Mechi 3)

Barcelona wamefunga mabao 1️⃣2️⃣ na kuruhusu mabao 2️⃣ tu.

🇪🇸

FULL TIME ⏰Aston Villa 0️⃣ ➖ 1️⃣ Arsenal⚽ 59' Bukayo Saka (🅰️ Calafiori)Arsenal anaendelea kusaka ubingwa wa EPL 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿...
31/08/2026

FULL TIME ⏰

Aston Villa 0️⃣ ➖ 1️⃣ Arsenal

⚽ 59' Bukayo Saka (🅰️ Calafiori)

Arsenal anaendelea kusaka ubingwa wa EPL 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 akiwa bingwa mtetezi.

🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when SokaOnline posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to SokaOnline:

Shortcuts

Share

Category