12/06/2020
EYMAEL Kumekucha Jangwani.
June 12,2020.
Akizungumza na BINGWA jana kutoka Shinyanga, Meneja wa timu hiyo, Abeid Mziba, alisema wamefanya mazoezi chini ya Charles Mkwasa, kwani kocha mkuu anatarajia kuungana na kikosi leo.
Alisema kati ya wachezaji waliokuwa wamebaki Dar es Salaam, kipa Metacha Mnata, amefika jana asubuhi na Bernald Morrison anaweza kufika leo.
“Tupo mazoezini jioni hii (jana) katika uwanja wa Fresho, kocha mkuu atakuwepo katika mazoezi ya kesho, Metacha amekuja na ndege ya asubuhi amewahi lakini pia Morrison atakuja asubuhi (leo),” alisema.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Msafara Dominic Albinus ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji alitaja sababu ya timu hiyo kufika alfajiri kuwa imetokana na changamoto walizopata njiani.
Albinus amezungumza na tofutti ya klabu hiyo, kuwa msafara wa timu hiyo ulichelewa baada ya gari yao kupata hitilafu ya kupasuka tairi ya mbele eneo la Manyoni mkoani Singida.
“Tumechelewa sana, lakini tunawashukuru sana wanachama na mashabiki wa Shinyanga ambao wametusubiri hadi alfajiri kutupokea, hii imetupa faraja kubwa na kwa wachezaji imewatia moyo,” alisema.