01/09/2026
RIZIKI YAKO HAIWEZI KUKOSEA ANWANI
September hii,usiingie kwenye biashara ukiwa na presha ya kutaka kila kitu kitokee kwa wakati ulioupanga
Kuna siku utauza sana,kuna siku utauza kidogo na kuna siku hutauza kabisa,usiruhusu siku ambayo haikuenda k**a ulivyotarajia ikufanye usahau mambo yote ambayo Mungu ameshakupa
K**a umeomba riziki, pia jifunze kushukuru hata kabla hujaiona kwa sababu sisi tunapanga lakini Mwenyezi Mungu ndiye anayejua wapi na lini riziki yetu itakutana nasi
Jukumu lako si kujua itakuja lini,jukumu lako ni kuhakikisha unapambana,unaweka juhudi na unatengeneza mazingira ya kukutana nayo
Mwezi mpya, moyo wa shukrani zaidi, kumbuka juhudi ni zako riziki ni ya Mungu ishi na hii
Uwe mwezi wa neema na baraka kwenye utafutaji wako,Mwenyezi Mungu akuongezee wateja zaidi kwenye biashara yako