28/01/2025
Katika maisha hauhitaji KUZIMA MSHUMAA WA MWENZAKO ili wa kwako ubakie unawaka. Hiyo ni roho mbaya. Na roho mbaya huwa ni risiti ya malipo ya baadae! Mafanikio hayakuhitaji uwaumize na kuwashusha watu wengine ili wewe ufanikiwe. Huo unakua ni uchawi tu k**a uchawi mwingine.
Kanuni za asili za ulimwengu zitakulipa sawa sawa na matendo yako. Hupendi kudhulumiwa basi usiwadhulumu watu wengine! Hupendi kudanganywa basi usidanganye! Hupendi kunafikiwa basi usiwanafiki wengine! Maisha ya hapa duniani yanakulipa sawa sawa na MATENDO YAKO.
Usiwe na tabia k**a za nyoka ambaye anaweza kugonga z**i zima la ng'ombe na kuwaua wote na wakati hawezi kumeza hata mguu mmoja wa ng'ombe! Sikiliza nikwambie, unapomharibia mwenzako kumbuka huo ni mkopo wenye riba, jiandae kuulipa Kwa gharama kubwa.
Ni sawa tu na kutema mate juu, lazima yakurudie! Epuka kuwafanyia watu UBAYA kwa kuwa huo ni mkopo utakao ulipa baadae kwa riba!
Wasiliana nami kwa elimu juu ya kujikubali na kujiamini kuwa mtu anayevuta mafanikio.
WA +255682147532