13/08/2026
Macho mbele Wana Simba wenzangu hii imeshapotea haikua rizki na hatuna sababu ya kulaumiana wala kutafuta mchawi
Kuna nyakati tulikua bora hatukutumia ubora huo kupata matokeo na kuna nyakati mpinzani wetu alikua bora akatumia ubora wake kupata matokeo
Tusikatishwe tamaaa wala tusijipoteze njiani, Tunayo safari muhimu sana mbele yetu Mechi 30 za ligi kuu
Nikiri tu kuwa Timu yetu inahitaji maboresho hasa kwenye eneo la ushambuliaji ndio eneo pekee mpaka saaa bado hatujafanya vizuri
Poleni Wana Simba wenzangu, Nguvu sasa tuielekeze kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi dhidi ya Kagera Sugar
Ally