21/07/2026
β
οΈππππ ππ’π‘π: YANGA YAMKAMILISHA USAJILI WA MSHUMBULIAJI HATARI JUSTICE FIGUAREIDO AKITOKEA CHIPPA UNITED
Klabu ya Young Africans imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Eswatini, Justice Johnpaul Figuareido, akitokea klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini.
Justice Figuareido ni mshambuliaji mwenye uwezo wa kucheza k**a winga wa kushoto, kulia au straika wa kati.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alianza safari yake ya soka nchini Eswatini kabla ya kuhamia Afrika Kusini ambako aliwahi kuzitumikia klabu za Maritzburg United, TS Galaxy, All Stars, Richards Bay na baadaye Chippa United. Pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Eswatini, akiwa ameichezea katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na kufunga mabao muhimu kwa taifa lake.
Ujio wa Figuareido unatarajiwa kuongeza ushindani mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya Yanga, huku benchi la ufundi likiamini uzoefu wake katika ligi yenye ushindani mkubwa k**a ya Afrika Kusini utakuwa silaha muhimu katika kampeni za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na kufanya vizuri katika michuano yakimatifa.
Follow