Liverpoolfc kopites Tanzania

Liverpoolfc kopites Tanzania Karibu kwenye ukurasa wa mashabiki wa Liverpool FC Tanzania. Tufollow usikose taarifa muhimu za liverpool....YNWA ❤️ |

Unaokuletea habari za usajili, mechi, matokeo, taarifa rasmi, mijadala na matukio mbalimbali yanayohusu Liverpool FC. Ukurasa huu ni kwamahususi kwa habari/mijadala/mada/ kutoka Timu ya liverpoolfc, Page hii inasimamia na kijana mtanzania shabiki wa Liverpoolfc, Page hii itatumia lugha ya kiswahili 99% ilikufikisha ujumbe kwa mashabiki wa Liverpoolfc wa hapa nyumbani na nje ya Tanzania zaidi ...

Lengo letu nikuwa pamoja k**a mashabiki na kufikishiana habari mbalimbali .. tumeamua kusimamia ili kuwatafutiti habari za timu yetu pendwa .... YNWA

🚨 Bradley Barcola kuhusu kujiunga na Liverpool:“Nilipojua kuhusu nia ya Liverpool kunisajili, sikuwa na maswali yoyote. ...
31/08/2026

🚨 Bradley Barcola kuhusu kujiunga na Liverpool:
“Nilipojua kuhusu nia ya Liverpool kunisajili, sikuwa na maswali yoyote. Nilijua moja kwa moja kwamba ilikuwa klabu kubwa sana kwangu.” 🔴✨
Maneno yanaonyesha jinsi ambavyo Bradley Barcola alivyoona nafasi ya kujiunga na Liverpool kuwa hatua kubwa katika maisha yake ya soka.

thisisanfield.com +1
**WELCOME TO LIVERPOOL, BARCOLA! 🔴🔥**

Mtazamo wako ? Dalili nzuri ipo msimu huu ?
29/08/2026

Mtazamo wako ? Dalili nzuri ipo msimu huu ?

🚨 TAARIFA: Mwanahabari wa Senegal, Khadim Diakhate, ameripoti kwamba Liverpool wanafikiria kuwasilisha ofa ya pili kwa a...
28/08/2026

🚨 TAARIFA: Mwanahabari wa Senegal, Khadim Diakhate, ameripoti kwamba Liverpool wanafikiria kuwasilisha ofa ya pili kwa ajili ya kumsajili Ismaïla Sarr. 🔴

Hii inamaanisha Liverpool wanaweza kuongeza dau lao baada ya ofa yao ya awali kutokukubalika.

🚨💣 BREAKING: LIVERPOOL WAMFIKIA MAKUBALIANO YA KUMSAJILI BRADLEY BARCOLA! 🔴Liverpool wamefikia makubaliano ya mdomo (ver...
27/08/2026

🚨💣 BREAKING: LIVERPOOL WAMFIKIA MAKUBALIANO YA KUMSAJILI BRADLEY BARCOLA! 🔴

Liverpool wamefikia makubaliano ya mdomo (verbal agreement) kumsajili Bradley Barcola kutoka PSG.

💰 Ada ya awali: £100m
💶 Package yote: Inaweza kufikia hadi €140m pamoja na add-ons.

📄 Nyaraka zinatarajiwa kubadilishana ndani ya masaa 24.

🎯 Barcola alikuwa target namba moja wa Liverpool kwenye dirisha hili la usajili — na sasa kila kitu kinaelekea kukamilika.

🔴 HERE WE GO! 🔥

Point Moja mfukoni, Mchezo dhidi ya Newcastle huwa ni mchezo mgumu sana siku zoteKwa mtazamo wako ni maeneo gani kuna ma...
23/08/2026

Point Moja mfukoni, Mchezo dhidi ya Newcastle huwa ni mchezo mgumu sana siku zote

Kwa mtazamo wako ni maeneo gani kuna mapungufu tunafaa tusajili haraka sana ili kuendana na Ligi

RASMI: CURTIS JONES AONDOKA LIVERPOOL! 💔Curtis Jones amekamilisha jana uhamisho wa kudumu kwenda Inter Milan, huku ukisu...
22/08/2026

RASMI: CURTIS JONES AONDOKA LIVERPOOL! 💔

Curtis Jones amekamilisha jana uhamisho wa kudumu kwenda Inter Milan, huku ukisubiriwa uthibitisho wa mwisho wa kimataifa.

Liverpool imemshukuru Jones kwa kujitolea kwake na mchango wake mkubwa kwa klabu katika kipindi cha miaka 16 tangu akiwa kwenye mfumo wa akademi hadi kufikia kucheza katika kikosi cha kwanza.

Baada ya miaka mingi akiwa sehemu ya familia ya Liverpool, Jones sasa anaanza ukurasa mpya wa maisha yake ya soka nchini Italia.

❤️ Asante kwa kila kitu, Curtis Jones.

Tunamtakia kila la heri na mafanikio katika sura mpya ya maisha yake akiwa na Inter Milan. 🔴

🚨🔴 BREAKING: LIVERPOOL WAMEFIKIA MAKUBALIANO NA YANKUBA MINTEH!Liverpool wamefikia makubaliano ya awali kwa njia ya mazu...
21/08/2026

🚨🔴 BREAKING: LIVERPOOL WAMEFIKIA MAKUBALIANO NA YANKUBA MINTEH!

Liverpool wamefikia makubaliano ya awali kwa njia ya mazungumzo (verbal agreement) na winga wa Brighton, Yankuba Minteh, huku klabu hiyo ikiwa tayari imewasilisha ofa rasmi ya £60 milioni ambayo hata hivyo imekataliwa na Brighton. 🔵⚪️

Mazungumzo kati ya Liverpool na Brighton yanaendelea, huku Minteh akionekana kuwa chaguo la ziada katika kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji, na si mbadala wa mchezaji anayelengwa zaidi na Liverpool, Bradley Barcola.

Liverpool bado wanaendelea na mpango wao wa kumsajili Barcola k**a kipaumbele, huku Minteh akiwa sehemu ya mipango ya kuongeza chaguo zaidi kwenye kikosi.

🔥 DEAL BADO INAENDELEA!
🔴 Liverpool wanataka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji kwa nguvu zaidi.

Mundo Deportivo inareport kwamba chaguo la kumnunua limewekwa kuwa €55M kwa Ronald Araujo, Liverpool inaripotiwa kufidia...
08/08/2026

Mundo Deportivo inareport kwamba chaguo la kumnunua limewekwa kuwa €55M kwa Ronald Araujo, Liverpool inaripotiwa kufidia 100% ya mshahara wake.

Kwa mujibu wa ripoti ya DaveOCKOP, ikinukuu mwandishi wa L'Équipe, Loïc Tanzi, Bradley Barcola ameripotiwa kukubaliana m...
05/08/2026

Kwa mujibu wa ripoti ya DaveOCKOP, ikinukuu mwandishi wa L'Équipe, Loïc Tanzi, Bradley Barcola ameripotiwa kukubaliana masharti binafsi ya mkataba na Liverpool. Hata hivyo, makubaliano kati ya Liverpool na PSG kuhusu ada ya uhamisho bado hayajakamilika, na ndiyo hatua muhimu iliyobaki kabla ya dili kukamilika.

BREAKING 🚨Real Madrid wameingia rasmi kwenye mbio za kuwania kumsajili Yan Diomande kutoka RB Leipzig, kwa mujibu wa Dav...
24/07/2026

BREAKING 🚨

Real Madrid wameingia rasmi kwenye mbio za kuwania kumsajili Yan Diomande kutoka RB Leipzig, kwa mujibu wa David Ornstein. Hii inaongeza ushindani mkubwa kwenye dili ambalo Liverpool wamekuwa wakilihusishwa nalo kwa kipindi chote cha dirisha hili la usajili, huku PSG ikitajwa kuwa ilikuwa inaongoza mbio hizo katika wiki za hivi karibuni.

Kwa sasa, mbio za Diomande zinahusisha vilabu vikubwa vya Ulaya, na hakuna makubaliano ya mwisho yaliyofikiwa. Liverpool bado wanatajwa kuwa miongoni mwa wanaomfuatilia kwa karibu, lakini sasa Real Madrid wameongeza presha kwenye vita ya usajili wake.

Address

Kunduchi
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Liverpoolfc kopites Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Liverpoolfc kopites Tanzania:

Shortcuts

Share

Category