23/11/2024
wa/call +255749961961
*•KIHARUSI (Stroke)*
🗣️Ugonjwa wa stroke humpata mtu ghafla na dalili hutokea kwa muda mfupi sana.Dalili kuu za ugonjwa huu ni:
✨ Kuchanganyikiwa,mtu akipata shida ya kuongea na kuelewa anachoambiwa
✨Maumivu ya kichwa yanakwenda pamoja na kupoteza fahamu kwa vipindi na kutapika
✨Ganzi katika viungo vya uso,mkono na mguu na hasa vikiwa vya upande mmoja wa mwili
✨Kupata shida ya kuona kwa jicho moja au yote
✨Kupata shida ya kutembea vikichanganyika na kizunguzungu na kukosa mpangilio wa matendo ya mwili
🗣️Athari za kiharusi zinaweza kuwa ni za muda mrefu. Kulingana na muda uliopita kabla ya kuugundua na kuutibu ugonjwa huu,mtu anaweza kupata ulemavu wa muda mfupi au wa kudumu.pamoja na madhara ya stroke k**a yalivyoorodheshwa hapo juu,mgonjwa wa stroke anaweza pia kupata yafuatayo:
⚡ Msongo wa mawazo
⚡Maumivu kwenye mikono na miguu yanayoongozeka baada ya viungo hivyo kufanya kazi au kutokea mabadiliko ya hali ya hewa.
⚡Kupooza au udhaifu wa upande mmoja wa mwili.