13/10/2017
..
MITAANI kuna kelele nyingi kuhusu kiungo, Jonas Mkude, kutoanzishwa kikosi cha kwanza pale Simba, huku wengine wakiona poa kwa vile Mghana James Kotei anafanya vizuri kwenye eneo la kati.
Lakini huko mazoezini wameliamsha. Kinachoendelea katika mazoezi ya Mnyama kuelekea mchezo wa keshokutwa Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar ni mpambano usio wa kawaida kati ya wachezaji hao wawili.
Viungo hao wamekuwa wakipambanishwa na kocha Joseph Omog, huku kila mmoja akionyesha vitu adimu ambavyo vimekuwa vikiwachanganya hadi wadau wa klabu hiyo kushindwa kujua nani mkali.
Katika tizi linalopigwa Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini, kocha amekuwa akiwapa kazi viungo hao kuonyesha umahiri wao hasa kutokana na ugumu wa mechi hiyo ambayo Mtibwa wameonekana kuipania.
Katika mazoezi ya juzi Jumatano jioni, Omog aliamua kugawa timu yake katika vikosi viwili; cha kwanza kikiundwa na Aishi Manula, Ally Shomary, Jamal Mwambeleko, Yusuf Mlipili, Salim Mbonde, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Said Ndemla, Juma Liuzio, Nicholas Gyan na Haruna Niyonzima.
Huku kikosi kingine kikiwa na akina Emmanuel Mseja, Erasto Nyoni, Mohammed Hussein, Method Mwanjali, Juuko Murshid, James Kotei, Jamal Mnyate, Mzamiru Yassin, John Bocco, Mohammed Ibrahim na Mwinyi Kazimoto.
Baada ya hapo akavipambanisha kwa muda wa dakika 40 na kazi kubwa ilionekana eneo la katikati kwa Mkude na Kotei kuonyeshana ushindani wa hali ya juu kila mmoja akitaka kumfunika mwenzake.
Wawili hao kila wakati walikuwa wakishindana katika kugombania mpira, kukaba na katika kuoneshana ufundi wa kupiga pasi ndefu na fupi jambo ambalo limeacha mtihani kwa kocha kwamba nani aanze.
Baada ya tizi hilo la nguvu.