07/03/2020
Sheria Namba 11 ya Mpira Wa Miguu Duniani,
11. KUOTEA
Ni kitendo cha mchezaji kuzidi au kupokea mpira akiwa mbele ya wachezaji wote Wa timu pinzani na akiwa ndani ya Eneo la timu pinzani .
– Mchezaji anaweza akawa katika nafasi ya kuotea lakini asitafsiriwe k**a ameotea k**a Hajajishughulisha kabisa na mpira .
– Dhana ya kuotea hutegemea mambo matatu muhimu ambayo ni Nafasi , kucheza na Kutoa .
– Pia mchezaji hatakuwa ameotea ikiwa walinzi Wa timu pinzani Watamkimbia au kutojishughulisha kabisa pale mchezaji Wa timu pinzani atakapo pokea mpira na kufunga goli .
– Mchezaji Hatatafsiriwa k**a ameotea akiwa amepasiwa na mchezaji wa timu pinzani kwa Kujua au Kutojua .
– pia , Ikiwa mchezaji yuko katika nafasi ya kuotea na mwenzake mwenye mpira akapiga mpira golini moja kwa moja bila kumpasia mpira huyo aliyeko katika nafasi ya kuotoa na kufunga goli , hapo mwamuzi attaruhusu goli bila kutafsiri Kuotea .
– Mchezaji atakuwa ameotea Iwapo mpira Utapigwa golini Ukagonga mlingoti mojawapo Wa goli au mlinda mlango na kurudi ndani ya Uwanja na kuguswa na mchezaji aliyekuwa katika nafasi ya Kuotea .
– Aidha , Hakutakuwa na dhana ya kuotea pale mchezaji atakapokutana na mpira Uliochezwa na mlinda mlango .
– Mpira Wa kurushwa Hauna kuotea , Pia mchezaji hatakuwa ameotea endapo atapokea mpira katika eneo lake kabla hajavuka Mstari Wa katikati ya Uwanja