29/08/2025
USHINDI MKUBWA ZAIDI WA BLUCE LEE
Muigizaji maarufu zaidi kuwahi kutokea
Bluce Lee aliwahi kusema kuwa moja ya ushindi mkubwa zaidi katika maisha yake ni ule alioushinda ugonjwa mkubwa uliokua unamuandama
Mnamo mwaka 1970 Bluce Lee aliumia vibaya mno uti wa mgongo alipokua akifanya mazoezi ya weightlifting nakupelekwa hospitali ambapo madaktari walimwambia kuwa inabidi aachane na sanaa ya uigizaji kutoka na tatizo ilo ambalo lilimlazimu kulala tu kwenye kitanda nakushindwa kusimama kwa muda wa miezi sita
Ndipo alipoamua kuanza kusoma vitabu mbali mbali zaidi ya vitabu 200 vya afya mwili na tiba za kisayansi nakuanza mpango maalumu wa mazoezi ambao ulimsaidia mpaka kuweza kusimama tena..
Funzo Haijalishi ni hali gani uliyonayo kwasasa lakini ukiweka juhudi nakutokata tamaa siku moja utainuka nakutimiza malengo yako hapa nazungumza na wale ambao wamekataa dhidi ya malazi mbali mbali nakuona kuwa mwisho wakutimiza ndoto zao umefika hapana jipe moyo simama tena nakuelekea ndoto zako..