12/10/2020
Ningelipenda kukuliza swali hili "
JE, WEWE NI DARAJA AU UKUTA KWA WATU WENGINE"
😢Hivi na wewe ni miongoni mwa wale wanaokwazika wengine wakifanikiwa.
🥺Wakipata mchumba unakasirika, wakinunua gari una nuna?
🥶Umo kwenye wale ambao hawapendi kuwaona wenzao wakiwazidi fedha, Uchumi, ujuzi.
😤Hupendi kuwaona wengine wakiwa na furaha?
Natumaini hauko hivyo.
Sote katika ulimwengu huu, tumeletwa kwa kusudi na k**a tukilitumikia shauri letu vizuri basi tunaweza kuishi maisha yenye furaha.
Tunapaswa kufanyika baraka kwa wengine na sio balaa. Kuwa madaraja na sio ukuta.
✍🏿 kuna watu wanaotusubiri tupige hatua katika maisha ili tufanyike daraja kwao, kufikia ndoto zao.
✍🏿 Ukilala ama kukata tamaa kuna maelfu ya watu nyuma wanakusubiri ufanyike daraja, ili na wao wafanyike daraja kwa wengine.
📒 Furaha yako na iwe katika kuijenga furaha ya watu wengine, tusimame kwa pamoja kuyafuta machozi ya wanaolia sasa, maana kesho watakapocheka watatukumbuka tulipokuwa pamoja nao taabuni.
Mabadiliko huanza na Fikra, Chukua hatua
Mafanikio yanaitaji subra na uvumilivu