29/04/2026
Swahili-Talk COCO-CARTOON
SEHEMU YA PILI: 𝐔𝐒𝐈𝐊𝐔 𝐖𝐀 𝐀𝐉𝐀𝐁𝐔 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐆𝐔𝐄𝐋
Lakini nyumbani hali ilikuwa tofauti…
Bibi Elena anataka Miguel afanye kazi za familia
Baba yake anataka awe mtoto wa nidhamu, si muimbaji.
Dada yake Sofia yeye anajali tu kula na kucheka 😂
Miguel akajikuta katikati ya vita:
👉 Ndoto yake VS familia yake
Siku moja usiku, akiwa peke yake, Miguel aliangalia gitaa lake, akasema:
“Kama sitafuata ndoto yangu… nitabaki nani?” 😔
Na hapo ndipo…
👉 safari ya ajabu kabisa ilipoanza…
Kuna siku moja tu inaweza kubadilisha maisha yako yote… na kwa Miguel, hii ndiyo siku yenyewe.
Ilikuwa ni usiku wa sherehe kubwa kijijini … watu walikuwa wanacheza, wanakula, wengine wanapiga stori k**a kawaida. Lakini kwa Miguel, huo haukuwa usiku wa kawaida.
Alikaa pembeni, akiwatazama watu wanavyofurahia muziki… moyo wake ukawa mzito 😔
Akasema kimoyomoyo: “Wao wanaruhusiwa kufurahia muziki… mimi kwanini sipaswi?”
Ghafla akili yake ikamwambia,
“Leo ndiyo siku ya kufanya maamuzi.”
Miguel akaamka taratibu, akaondoka kimya kimya k**a mwizi wa kuku 😂
Akaelekea mahali palipokuwa na picha ya msanii wake mkubwa aliyekuwa anamkubali sana.
Alisimama mbele ya picha ile, macho yake yakiwaka k**a taa ya tochi
Akasema:
“Kama kweli nina kipaji… basi leo lazima nithibitishe!”
Pale karibu kulikuwa na gitaa ya zamani sana… ya kuvutia k**a ina historia ya ajabu.
Miguel akaisogelea taratibu…
“Mmmh… hii si gitaa ya kawaida…”
Lakini kwa kuwa ndoto zilikuwa zimemjaa kichwani, hakujali sana. Akaishika, Akaipiga mpigo mmoja…
“TING!!!” 🎸
Ghafla… dunia ikabadilika 😳
Upepo ukavuma kwa nguvu 🌪️
Mwanga wa ajabu ukaanza kuzunguka kila upande...
Miguel akasema kwa mshangao:
“Hii nini tena?!
Alipofungua macho vizuri…
Alijikuta mahali ambapo si pa kawaida kabisa…
Watu waliokuwa wanatembea pale hawakuwa watu wa kawaida…Walikuwa ni mifupa! 💀💀
ITAENDELEA.
Follow page yetu Swahili-Talk