albinismsports

albinismsports Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from albinismsports, Sports Club, Kinondoni, Manyanya. . near Osha office, Dar es Salaam.

Albinism Sports and Culture Tour is a programme established for the purpose of raising awareness of the community to get better understanding of albinism and the challenges facing persons with albinis

11/06/2026

Katibu Mkuu wa ASC ndg Joseph Sinda aelekea Tarime kwa ajili ya maandalizi ya Siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa juu ya Ualbino (International Albinism Awareness Day) yatakafika Tarehe 13 juni 2026 wilayani Tarime Mkoa wa Mara

08/06/2026

Uongozi wa Albinism Sports Club unatuma salamu za rambirambi kwa familia ya Makunda na mchezaji wao ndugu Jofray Makunda kwa kufiwa na dada yake Joyce Makunda.

ASC walipokea kwa huzuni taarifa ya msiba wakiwa Dodoma pamoja na mchezaji wao Jofray Makunda ambae ni mdogo wa marehemu wakati wakijiandaa na mechi maalum na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Bunge Sports Club) ni huzuni kubwa sana.

Mungu awape nguvu, uvumilivu,na amani katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu. Tunawaombea faraja na roho ya utulivu. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi."

05/06/2026

Kilabu ya Michezo ya Watu wenye Ualbino (Albinism Sports Club) kwa umoja wao jana tarehe 05/06/2026 walishuhudia Bunge mubashara (live).

Hatua moja huamzisha nyingine haikuwa kazi rahisi.

Pongezi nyingi sana kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na uongozi mzima wa Bunge kwa kuonyesha kuwajali na kuwathamini Watu wenye ulemavu wakiwemo Watu wenye Ualbino hii ni hatua moja mbele kwa ASC kuonekana na kutambuliwa kuwa nao wapo na wanathaminiwa. kuonekana Bungeni kutaendelea kuleta chachu kwa jamii kuwashirikisha Watu wenye Ualbino katika shughuli mbalimbali za kiuchumi, Kijamii na kisiasa ikiwemo michezo na hilo ndio moja ya lengo la ASC.

Kila jambo lina wakati wake yote haya ni matokeo ya kuwezeshwa na Baraza la michezo la Taifa (BMT) likiongozwa na Dada yetu Neema Msitha na timu yake bila wao ASC isingefika hapa.

Wito kwa Wakazi wa Dodoma na maeneo ya jirani kuja leo kushudia mtanange kabambe kati ya Bunge Sports Club na Albinism Sports Club katika uwanja wa Jamhuri Dodoma kuanzia saa 10:00 jioni kabla ya mechi kutatanguliwa na shughuli mbalimbali ikiwemo semina ya afya na mazingira.

Karibu wote mjulishe na mwenzako. Asikose kushudia Wachezaji wenye Ualbino wanavyocheza matata mimpira na kuwafunga magoli mengi Bunge Sports Club.


05/06/2026

Wachezaji wa Albinism Sports Club wakiwa na viongozi wao pamoja na wadau wao leo asubuhi saa 02:00 kamili watatembelea. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hii itafanyika kabla ya Bonge la mechi kali kati ya timu ya Bunge Sports Club Vs Albinism Sports Club mechi itakachezwa kesho tarehe 06/06/2026 saa 11:00 jioni katika uwanja wa Jamhuri Dodoma. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Paul Makonda .

Pongezi nyingi sana kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Mhe Dr Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya habari utamaduni sanaa na michezo ikiongozwa Mhe Paul Makonda ambayo imeipa jukumu Baraza la michezo la Taifa kuendeleza michezo Kwa kweli wanawajali na kuwathamini Watu wenye Ulemavu Tanzania

Kwa kipekee ASC inalipongeza sana Baraza la michezo la Taifa likiongozwa na Katibu Mtendaji Dada Neema Msitha na timu yake nzima kwakuwa ndio wameifungulia njia ASC mpaka hapa ilipo inaanza kupata fursa mbalimbali zinazotokana na michezo Kwa mfano leo ASC wanaingia Bungeni na kesho wanacheza mechi ya mpira wa Miguu na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bunge Sports Club hii ni fursa adimu sana Pongezi nyingi sana kwao.

Pia ASC inatuma shukurani zake nyingi sana kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likiongozwa na Mheshimiwa Azzan Zungu kwa kukubali kucheza mechi ya kirafiki na kuwakaribisha kutembelea Bunge hii italeta chachu na hamasa kwa jamii kuona kwa kuwa Watu wenye Ualbino Wana haki sawa na wanashirikishwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi, Kijamii na kisiasa ikiwemo michezo.

Wito kwa Wakazi wa Dodoma na maeneo ya jirani kujitokea kwa wingi kushudia mtanange huo mkali pale uwanja wa Jamhuri kesho tarehe 06/06/2026 kuanzia Saa 11:00 jioni lakini pia kutatanguliwa na shughuli mbalimbali ikiwemo semina ya kuhusu afya ya ngozi utunzaji wa mazingira n.k

Karibuni sana.


sbu







@

19/05/2026

Katibu Mkuu wa ASC ndg Joseph Sinda aeleza kuwa Mbio ya Kimataifa ya kuongeza uelewa juu ya Ualbino (International Albinism Awareness Marathon season 1 2026) ni Mbio jumuishi itawahusisha Watu wote wenye Ualbino na wasio kuwa na Ualbino wakiwemo wakubwa kwa wadogo kwa hiyo wote mnakaribishwa kushiriki bila kukosa unaikosaje kwa mfano.

Mbio hiyo itafanyikia Mkoa wa Mara wilaya ya Tarime tarehe 13 juni 2026 pia wataadhimisha siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa juu ya Ualbino. Kwa kushirikiana na Shirika la Tramepro siku hiyo na watashiriki kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya umma k**a Shule,Stendi, Hospitali.

Kwa wanaopenda kushiriki wawasiliane na katibu Mkuu 0747489804 au email [email protected] ili kupata fomu na maelezo zaidi.




tanzania







14/05/2026

Katika Mbio hiyo ya Albinism awareness international Marathon ASC wanatarajia kuwaalika pia waheshimiwa wabunge ili kuhakikisha mbio inakuwa na mvuto wa hali ya juu kwaku ndo Mbio ya kwa kufanyika Duniani.

Pia wanatara kumualika Mhe Paulo Makinda kuwa mgeni rasmi baada ya kukamilishamahitaji.

Ungana nao kwa no nao siku hiyo

Kwa kuchangia my ulichobarikiwa wezesha kupitia lipa namba Mpesa 50613388 au akaunti no Ndani ya kipindi cha kambi ya michezo ITV/Radio One tarehe 13/05/2026 ambapo Katibu Mkuu wa Albinism Sports Club Ndg Joseph Sinda alishiriki kufanyiwa mahojiano na mtangazaji wa habari za michezo Ndg Khalid Msabaha.

Hii ni kuelekea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa juu ya Ualbino na kujiandaa na Mbio ya kimataifa ya kuongeza uelewa juu ya Ualbino (International Albinism Awareness Marathon 2026.

Hii ni kwa mara ya kwanza kufanyika Duniani itakayofanyika Wilayani Tarime Mkoani Mara tarehe 13/06/2026

Lengo la Marathon hiyo ni
1. kuendelea kuelimisha jamii juu ya Ualbino
2. Kuwezesha upatikanaji wa mahitaji mbalimbali na fedha za ujenzi wa Uzio wa Shule ambayo Watoto wenye Ualbino wanayosoma ili wawe katika mazingira salama.
3. Kujenga kituo cha michezo na uwanja wa kisasa shirikishi wa michezo kwa Watu wenye Ualbino na wasio na Ualbino.
4. Kuwezesha upatikanaji wa fedha za kuanzisha miradi mbalimbali endelevu itakayowawezesha Watu wenye Ualbino wenye vipaji na wasio na wasio na vipaji ili kuondokana na uchumi tegemezi ambao ndio chanzo kikuu cha ubaguzi,unyanyapaa, naukatili dhidi ya Watu wenye Ualbino.

Ungana nao kwa kukimbia nao pamoja kuonyesha upendo kwao.

Wezesha Mbio hiyo kwa kuchangia chochote ulichobarikiwa kwenda lipa Mpesa 50613388 au kwenye akaunti no
20510066242 jina Albinism Sports Club.

14/05/2026

Ilikuwa mubashara (live) katika kipindi cha kambi ya michezo ITV/Radio 📻 One ambapo Katibu Mkuu wa Albinism Sports Club alishiriki mahojiano na mtangazaji wa habari za michezo Ndg Khalid Msabaha.

14/05/2026

Ndani ya kipindi cha kambi ya michezo ITV/Radio One tarehe 13/05/2026 ambapo Katibu Mkuu wa Albinism Sports Club Ndg Joseph Sinda alishiriki kufanyiwa mahojiano na mtangazaji wa habari za michezo Ndg Khalid Msabaha.

Hii ni kuelekea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa juu ya Ualbino na kujiandaa na Mbio ya kimataifa ya kuongeza uelewa juu ya Ualbino (International Albinism Awareness Marathon 2026.

Hii ni kwa mara ya kwanza kufanyika Duniani itakayofanyika Wilayani Tarime Mkoani Mara tarehe 13/06/2026

Lengo la Marathon hiyo ni
1. kuendelea kuelimisha jamii juu ya Ualbino
2. Kuwezesha upatikanaji wa mahitaji mbalimbali na fedha za ujenzi wa Uzio wa Shule ambayo Watoto wenye Ualbino wanayosoma ili wawe katika mazingira salama.
3. Kujenga kituo cha michezo na uwanja wa kisasa shirikishi wa michezo kwa Watu wenye Ualbino na wasio na Ualbino.
4. Kuwezesha upatikanaji wa fedha za kuanzisha miradi mbalimbali endelevu itakayowawezesha Watu wenye Ualbino wenye vipaji na wasio na wasio na vipaji ili kuondokana na uchumi tegemezi ambao ndio chanzo kikuu cha ubaguzi,unyanyapaa, naukatili dhidi ya Watu wenye Ualbino.

Ungana nao kwa kukimbia nao pamoja kuonyesha upendo kwao.

Wezesha Mbio hiyo kwa kuchangia chochote ulichobarikiwa kwenda lipa Mpesa 50613388 au kwenye akaunti no
20510066242 jina Albinism Sports Club.

13/05/2026

Tarehe 13 Mei 2026 Katibu Mkuu wa Albinism Sports Club Ndg Joseph Sinda atakuwa mubashara (Live) katika kipindi cha kumekucha ITV kuanzia saa 02:00 asubuhi kuzungumzia Mbio ya kimataifa ya kuongeza uelewa juu ya Ualbino (Albinism Awareness International Marathon 2026) kwa mara ya kwanza kidunia itafanyikia Mkoa wa Mara wilaya Tarime tarehe 13/06/2026 pia itaendana na maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa juu ya Ualbino (International Albinism Awareness Day 2026).

Lengo kuu la Mbio hiyo ni
1. kuendelea kuelimisha jamii juu ya Ualbino.
2. Kuwezesha kuendesha harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa Uzio wa Shule ambayo w Watoto wenye Ualbino watasoma kwa usalama, ujenzi wa kituo cha michezo

Pia Mbio hiyo itakuwa sehemu ya kuvitangaza vivutio mbalimbali vilivyoko Wilaya ya Tarime, Wilaya zinazopana nayo na
Tanzania kwa ujumla sambamba na kuongeza mapato kwa kuwa wageni watakaoshiriki watatokea nchi mbalimbali za Ulaya, America na Asia 🌏.
Kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dr Samia Suluhu Hassan kutangaza utalii wa ndani na nje kwa kutembelea mbuga na vivutio mbalimbali vilivyoko Kanda ya ziwa , kaskazini na maeneo ya jirani kulingana na uwezesho utakaokuwepo.

Ungana nao kwa kukimbia nao pamoja kuonyesha upendo kwao Kwa kushiriki jisajili Sasa.

Wezesha Mbio hiyo kwa kuchangia chochote ulichobarikiwa kupitia lipa Mpesa 50613388 au akaunti no 20510066242 jina ni Albinism Sports Club.

Kwa maelezo zaidi piga 0747489804 au email [email protected]







tanzania












matiko







online.news
tanzania





Tarehe 13 Mei 2026 Katibu Mkuu wa Albinism Sports Club Ndg Joseph Sinda atakuwa mubashara (Live) katika kipindi cha kume...
12/05/2026

Tarehe 13 Mei 2026 Katibu Mkuu wa Albinism Sports Club Ndg Joseph Sinda atakuwa mubashara (Live) katika kipindi cha kumekucha ITV kuanzia saa 02:00 asubuhi kuzungumzia Mbio ya kimataifa ya kuongeza uelewa juu ya Ualbino (International Albinism Awareness Marathon 2026) kwa mara ya kwanza kidunia itafanyikia Mkoa wa Mara wilayani Tarime tarehe 13/06/2026 pia itakuwa ni maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa juu ya Ualbino (International Albinism Awareness Day 2026).

Ungana nao kwa kukimbia nao pamoja kuonyesha upendo kwao Kwa kushiriki jisajili Sasa .

Wezesha Mbio hiyo kwa kuchangia chochote ulichobarikiwa kupitia lipa Mpesa 50613388 au akaunti no 20510066242 jina ni Albinism Sports Club

Kwa maelezo zaidi piga 0747489804 au email [email protected]

Address

Kinondoni, Manyanya. . Near Osha Office
Dar Es Salaam

Telephone

+255767212428

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when albinismsports posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to albinismsports:

Share

Category