19/08/2023
.
βπ»Kipindi cha kwanza hizi timu mbili zilionesha udhaifu wa hali ya juu sana kwenye maeneo mengi
1: Uzuiaji mbaya sana
2: Pressing ambayo haina uimara
3: Mipira kupotea kirahisu sana
4: Kushindwa kumiliki mchezo hasa kwa wale viungo 6 wote ni Bissouma pekee ndio alikuwa anaonesha uhai
5: Umaliziaji duni
βπ»Spurs kwenye muundo wao mpya wa 2-3-5 , fullbacks wawili wanaingia ndani mstari mmoja na Bissouma huku Maddison na Sarr wakiwa namba 8 wawili , kwenye uanzishaji wao wa mashambulizi hasa kipindi cha kwanzw haikuwa nzuri sana na kufanya hata pressing ya United kuonekana nzuri sana ambapo walikuwa wana press na 4-1-4-1 maana yake United walizuia njia zote za pasi kwenda katikati
βπ»United walikuwa wanakosa control , wapo direct sana matokeo yake wanapoteza mipira kirahisi
1: Hakuna muunganiko mzuri baina ya mabeki wa kati na kiungo namba 6 wa United
2: Hakuna muunganiko mzuri baina ya namba 6 na namba 8 wawili wa United
3: Baada ya hapo United wakipoteza tu mpira , Rashford anakuwa k**a kapewa kadi nyekundu , hana msaada kwenye kuweka presha kwenye mpira
βπ»Kipindi cha pili Spurs walionesha njaa zaidi kuliko United , walipasia mpira vizuri , walishambulia vizuri , build up nzuri sana kuliko United , na hata level ya kuzuia ilikuwa nzuri kuliko kipindi cha pili . Timu bora uwanjani hasa kipindi cha pili ndio imeshinda mechi
NOTE
1: Yves Bissouma aliwavurga sana Man United , kuanzia filimbi ya kwanza mpaka ya mwisho
2: Vicario golini , saves katika nyakati sahihi
3: Level ya uimara wa kimwili kwa baadhi ya wachezaji wa United na Spurs inatia wasiwasi sana ( Varane kwenye kasi ? π€ Casemiro huruma , Van De Ven wa Spurs k**a anatembea )
4: Ukiondoa tena Onana leo unaangalia wachezaji waliobaki wa United unashika kichwa π€
5: Mechi yake ya pili Ange Postecoglou lakini unaona nini Spurs wanajaribu kufanya lakini unajiuliza ETH nini anajaribu kufanya mpaka sasa ? π€
By mchambuzi George Ambangile