19/01/2023
Kuna wakati mambo yanaenda vizuri upande wako kila unachogusa ni uhakika mpaka unajihisi ni mbarikiwa k**a Yakobo mwana wa Isaka
Alafu upo ule wakati kila kitu kwako ni mtihani 1 haikai wala 2 haifai! Kazini matatizo, mahusiano hayaeleweki, ndugu wanaleta noma, watu unao amini ni msaada hawapokei simu wala kujibu text mpk unadhani duniani umekuja kuteseka
Ugumu wa maisha ndio kitu pekee kinachofanya watu wengine waishi, yupo ambae hajui atakula nn lkn yupo mtu anakula na kusaza kinabaki anamwanga, maana halisi ya Tuishi
Bahati mbaya sana tunaogopa nyakati ngumu kuliko kitu chochote, tunasahau hiki ni kipimo cha ukomavu, imani ya ushindi ikawe na ww k**a vile Mfalme Daudi dhidi ya Goliathi, Daniel dhidi ya simba wenye njaa kali au Shadraka, Meshaki na Abednego katika tanuru la moto mkali
Believe Yourself, Fanya kazi kwa bidii, usitamani cha mwingine, subiri wakati wako wa baraka ukufikie hayupo ambae Mungu amemsahau kila mmoja wetu anakusudio la kuwepo hapo alipo
We'll overcome more than overcome in him who strengthens us
Mkweli Alcantara noted by