Elcapitano Maestro

Elcapitano Maestro 1️⃣. Sports Pundit (English & Swahili) 2️⃣. i'm the best football analyst in africa

DARASA HURU  💁🏾‍♂️Mwandishi 🗣️ "Unafikiri ni nani atashinda Ballon d'Or mwaka huu 2026..?"Rais wa Laliga Javier Tebas 🗣️...
02/09/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Mwandishi 🗣️ "Unafikiri ni nani atashinda Ballon d'Or mwaka huu 2026..?"

Rais wa Laliga Javier Tebas 🗣️ "Rodri amekuwa nje ya soka ya klabu kwa muda mrefu kutokana na jeraha la misuli ya paja lakini amecheza vizuri kwenye Kombe la Dunia na kushinda tuzo ya mchezaji bora.

Kwa hivyo Rodri anastahili Ballon d'Or nyingine🏆🇪🇸"

💁🏾‍♂️

DARASA HURU 💁🏾‍♂️JE MALENGO NI YAPI...?Elcapitano Maestro 🗣 Kila klabu ina malengo yake ambayo inatamani kuyatimiza kwa ...
02/09/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

JE MALENGO NI YAPI...?

Elcapitano Maestro 🗣 Kila klabu ina malengo yake ambayo inatamani kuyatimiza kwa msimu huu 2026-27.

1️⃣. ARSENAL - Kutetea ubingwa ndilo dhumuni lake namba moja, maana ukiwa bingwa sheria namba 1 ni kujaribu kuutetea ubingwa wako kwa gharama yoyote.

Kikosi chao bado kipo imara sana lakini arteta anatakiwa awe makini sana katika kuamua nani sahihi wa kuanza katika eneo la namba 9.

Kuna aina ya wachezaji huwa wanakuwa na form nzuri sana ikiwa hawatafanyiwa sana rotation.

Kumtegemea Havertz ili akupe ubingwa wa ligi ni k**ari ambayo kuna muda utahitaji maombi sana ili iweze kutimia.

Kuna namna ambavyo arteta hajaridhishwa na Gyökeres lakini yeye ndie mfungaji bora zaidi kwa Arsenal 2025-26.

Mikel Arteta anapaswa kuwa makini sana kombe la ligi sasa limekuwa wazi zaidi.

2️⃣. MANCHESTER CITY - Usajiri mkubwa walioufanya ni kwa ajiri ya kuwania ubingwa wa ligi.

Man City kwenda zaidi ya misimu miwili bila kuchukua ubingwa ni japo ambalo halijawahi kutokea kwa msimu 9 mfululizo.

Hivyo wanaona wana kiu ya kuwania ubingwa na kurudisha ufalme wao.

3️⃣. LIVERPOOL - Ni mabingwa wa ligi msimu juzi maana Arsenal ndio waliomvua ubingwa.

Hivyo kuanguka msimu mmoja sio sababu ya kuwatoa katika kuwania mbio za ubingwa.

Msimu jana walijaribu kufanya usajiri wa nguvu ili kujaribu kutetea ubingwa lakini haukuleta matokeo.

Msimu huu wapo katika kujaribu kulirudisha kombe ambalo waliwahi kuwa nalo msimu juzi.

Japo upinzani ni mkali sana.

4️⃣. CHELSEA - Lengo lao ni kurejea katika michuano ya Uefa champions league.

Huwezi kuwadai ubingwa kwasababu chelsea hawakuwa na muendelezo wa kufanya vizuri kwenye ligi.

Ikiwa wachezaji wataamua kucheza kufa kupona kwa ajiri ya ligi hio ndio itaenda kuzaa malengo makubwa zaidi kwao.

5️⃣. Manchester United - wameboresha kikosi kwa ajiri ya ligi na uefa champions league huo ndio mtazamo wao.

Lakini ikiwa watakosa ubingwa haitakuwa stori kubwa k**a wao kuweza kufika fainali ya uefa champions league.

Man united bado wanahitaji muendelezo wa kufanya vizuri kwa kikosi chao wakiamua kukaza kwenye ligi bado watakuwa na uwezo wa kufanya vizuri kwenye ligi.

💁🏾‍♂️

DARASA HURU 💁🏾‍♂️SUBIRA NDILO DARAJA LA KUUPATA UKWELI KAMILI.Elcapitano Maestro 🗣 si kwamba iniesta ni mchezaji mkali s...
02/09/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

SUBIRA NDILO DARAJA LA KUUPATA UKWELI KAMILI.

Elcapitano Maestro 🗣 si kwamba iniesta ni mchezaji mkali sana kuliko Jude Bellingham japo namba zinataka kujaribu kuleta mjadala lakini hapana ili Jude aweze kulinganishwa na Iniesta atahitaji muda wa kufanya mambo makubwa.

Iniesta ni mchezaji mkali dhidi ya Jude lakini si mchezaji mkali sana kushinda Jude.

ipo hivi...👇

Iniesta ni k**a profesa ambae ana miaka 15 ya kufundisha soka wakati Jude ni profesa mwenye miaka 2 tangu aanze kazi hio.

Kwa aliyoyafanya Iniesta kwa miaka 15 inapelekea kuwa mchezaji mkali dhidi ya Jude.

Baada ya miaka 10 ukweli utachukua nafasi yake ya kujua nani bora zaidi kati ya Iniesta au Jude Bellingham.

Kwa wakati huo ndio tutajua kwamba k**a Iniesta ni mchezaji mkali sana kuliko Jude au laah.

Kuna wakati ili uupate ukweli kamili lazima muda kwanza upite, subira ndilo daraja la kuupata ukweli.

💁🏾‍♂️

DARASA HURU 💁🏾‍♂️Gabriel Jesus 🗣️ "Nilikubali mshahara mdogo kuja Barcelona kwa sababu ningependelea kuichezea Barcelona...
01/09/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Gabriel Jesus 🗣️ "Nilikubali mshahara mdogo kuja Barcelona kwa sababu ningependelea kuichezea Barcelona kuliko pesa nyingi.

Sikutarajia kuja hapa, kwa hivyo nadhani Mungu amechagua kwa ajili yangu. Sikuja kuiimarisha Barca kwa sababu ni timu imara tayari bali nimekuja kuwasaidia kadri niwezavyo."

nb: Elcapitano Maestro 🗣 barca itatumika k**a daraja kwa Gabriel kwenda kumalizia soka lake uarabuni na kuvuta mkwanja mrefu huko.

k**a Ferran Torres amefanikiwa kwenda PSG na hakuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza, hata Gabriel nae nafasi anayo.

Kuna muda kuanza kazi kwa mshahara mdogo si kwamba unajisaliti, itumue leo kuijenga kesho yako.

Karibu Barcelona Gabriel Jesus, japo sisi wadau wa Barca tuna tamani siku moja kumuona Mikel Arteta akirudi nyumbani Barcelona, uzuri hili hata arteta analijua 😀.

💁🏾‍♂️

DARASA HURU 💁🏾‍♂️LIONEL MESSI AMEAMUA KUACHANA NA SOKA LA KIMATAIFAElcapitano Maestro 🗣 Jana usiku soka lililia leo asub...
01/09/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

LIONEL MESSI AMEAMUA KUACHANA NA SOKA LA KIMATAIFA

Elcapitano Maestro 🗣 Jana usiku soka lililia leo asubuhi tuliamka na ukweli, hatutamwona tena namba 10 wa Argentina.

Mazoea ndio kitu ambacho kitawaumiza zaidi mashabiki wa Lionel Messi na wapenda soka duniani kote.

Lionel Messi aliibeba taswira ya Argentina 🇦🇷 miaka 18, tumezoea kumuona akicheza kila pale ambapo anahitajika na taifa hilo.

Na sasa Lionel Messi amefikia ukomo wa kutoendelea kulichezea taifa lake la Argentina.

NAMBARI ZINAZIONGEA..

Akiwa na Timu ya Taifa ya Argentina 🇦🇷

Mechi 230.
Magoli 141.
Kombe 1 la Dunia.
Copa 2.
Finalissima 1.
Ballon d'Or 8.

Ameamua kuachana na Argentina huku yeye akiwa k**a mfungaji bora zaidi wa taifa hilo.

Hii sio CV bali ni HISTORIA.

Lionel Messi anaacha kuichezea timu ya taifa huku ndoto yake ikiwa imetimia.

Kipindi akiwa kijana mdogo aliulizwa malengo yake kwenye mpira wa miguu ?

Lionel Messi alijibu 🗣 "Ndoto yangu ni kucheza katika taifa la Argentina na kushinda kombe la dunia k**a Diego Maradona."

Hatimae ndoto yake imekamilika na akashinda zaidi ya Maradona na akatupa kumbukumbu isiyofutika.
..2022, kabla ya kombe la dunia kuanza kwa mwaka huo, mimi Elcapitano Maestro nilisema kwamba Argentina 🇦🇷 wataenda kutwaa kombe la dunia kitu ambacho wengi hawakuamini lakini ikawa kweli.

Kila la kheri Lionel Messi, Asante kwa kila usiku uliotufanya tusahau matatizo yetu kwa dakika 90.

💁🏾‍♂️

DARASA HURU 💁🏾‍♂️KIKOSI BORA KWA KILA MWEZI NI KIOO KWA LIGI.Elcapitano Maestro 🗣 kuna faida kadhaa za kuwepo kikosi bor...
01/09/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

KIKOSI BORA KWA KILA MWEZI NI KIOO KWA LIGI.

Elcapitano Maestro 🗣 kuna faida kadhaa za kuwepo kikosi bora cha kila mwezi kwenye ligi lakini leo nitawapa sababu 5.

1️⃣ INAWAPA MOTIVATION WACHEZAJI

Mchezaji anapojua k**a atacheza vizuri Septemba ataingia kwenye kikosi bora hio inampa chachu na motisha ya kupambana zaidi.

2️⃣ INAUZA LIGI

Wakati NBC inatangaza kikosi bora wapo wadau wataongea sana na kujadili, kwa mfano mbona huyu kaingia na huyu hapana? hii itamsaidia mchezaji kuanza kujulikana kwa urahisi zaidi.

Kitu k**a hii inavutia wadhamini,na hata scouts kutoka nje kwasababu Ligi inaonekana ni hai.

3️⃣ INAWASAIDIA MAKOCHA KUONA FORM YA MCHEZAJI MMOJA MMOJA.

Mfano kocha wa Yanga anatafuta striker ataanza kuangalia kikosi bora mwezi nani kaingia mara nyingi.

Mchezaji kuingia katika kikosi ch mwezi ni mfano wa CV kwake...

4️⃣ INATOA HESHIMA KWA WACHEZAJI WADOGO

Sio Yanga na Simba tu hata kwa wachezaji wa timu zingine wakicheza vizuri nao watapata nafasi ya kuingia kwenye kikosi bora kwasababu namba zinaongea.

Hii itasaidia kuonesha kwamba ligi yetu haina ubaguzi na kila mtu ana nafasi.

Shabiki ataangalia timu yake tu lakini bodi na k**ati ya ligi itafatilia timu zote.

5️⃣ INAANDIKA HISTORIA YA LIGI

Baada ya miaka 5 utakumbuka: "Septemba 2025 kikosi bora cha mwezi kiliundwa nani na nani.

Inakuwa kumbukumbu k**a 'Team of the Season" ila kwa haraka.

Nb: mlete na mwenzio aje kujifunza soka hilo ndilo lengo la Elcapitano Maestro.

Shabiki ataangalia timu yake tu lakini Elcapitano Maestro anaangalia ligi nzima.

💁🏾‍♂️

DARASA HURU 💁🏾‍♂️FT: ASTON VILLA  0 - 1 ARSENALElcapitano Maestro 🗣 baada ya mechi hii kumalizika kuna shabiki wa arsena...
01/09/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

FT: ASTON VILLA 0 - 1 ARSENAL

Elcapitano Maestro 🗣 baada ya mechi hii kumalizika kuna shabiki wa arsenal alinicheki kwenye Gmail yangu.

Shabiki wa Arsenal 🗣 mbona k**a Arsenal wamechoka sana maana vile ambavyo nilitegemea arsenal wangecheza labda kwa kasi sana na mashambulizi mengi lakini imekuwa tofati shida ni nini?

Elcapitano Maestro 🗣Nikamjibu 👇 ngoja niwawekee kwa kiswahili.

1️⃣.Arsenal ni bingwa mtetezi na anaonesha ana nia ya kutetea angalia hata wachezaji aliokuwa nao na aliowaongeza pia, angalia anatoka Skelly kisha anaingia Guimarães.

2️⃣.Arsenal haitafuti matokeo kwa kucheza ili amfurahishe shabiki, wao kupata alama tatu ni jambo bora kuliko kuhangaika timu ishinde kuanzia mabao 3+

3️⃣.Mechi ambazo anajua zina presha, Arsenal huwa anakuwa mtulivu zaidi na kucheza kwa tahadhari.

Tahadhari ya Arsenal wala si udhaifu, ndomana umeweza kuona Aston Villa kwenye mechi hakuwa na On Target hata yeye Arsenal alikuwa na on target 2 tu.

Huenda Aston Villa alikuwa anataka acheze na Arsenal kwa kupishana sana lakini Arsenal walikuja na mpango tofauti.

Shabiki wa Arsenal 🗣 Je, unadhani Arsenal tunaweza kutetea ubingwa wetu...?

Elcapitano Maestro 🗣..................nilimjibu.

💁🏾‍♂️

DARASA HURU 💁🏾‍♂️ROBERT SANCHEZ KWENDA COMO KWA UHAMISHO WA MKOPO AKITOKEA CHELSEA.Elcapitano Maestro 🗣 Baada ya Chelsea...
31/08/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

ROBERT SANCHEZ KWENDA COMO KWA UHAMISHO WA MKOPO AKITOKEA CHELSEA.

Elcapitano Maestro 🗣 Baada ya Chelsea kumsaini Emiliano Martinez, klabu kadhaa barani ulaya ziliibuka na kumtaka Robert Sanchez.

Chelsea sasa wana Martinez, je wana ulazima gani wa kumtoa kwa mkopo Sanchez badala ya kumuuza moja kwa moja 😀...?

Nadhani Chelsea wenyewe wanajua shida ya klabu yao ipo wapi kuliko mashabiki wao wanavyodhani.

ila kwa anaejua mpira huwezi kutofautisha ubora wa Emiliano Martinez na Robert Sanchez.

Emiliano Martinez alishinda kombe la dunia akiwa na Lionel Messi dhidi ya Ufaransa timu bora sana kwa wakati huo na yenye mbappe.

Pia Martinez alishinda golikipa bora wa michuano hio.

Robert Sanchez alishinda Club World Cup dhidi ya PSG ambayo ni bora zaidi duniani na yenye mchezaji bora zaidi wa dunia kwa wakati huo na ilikuwa na nyota wengi pia.

Pia Robert Sanchez alishinda golikipa bora wa michuano hio.

Martinez na Sanchez ni magolikipa wanaoweza kufanya saves nyingi wanafanana katika hilo na kwenye makosa wanafanana pia.

Psychologically watu wanampa heshima zaidi Martinez labda kwasababu ya kombe la dunia lakini kwa ufundi bado ni 50-50.


💁🏾‍♂️

DARASA HURU 💁🏾‍♂️ILIMAN NDIAYE KUJIUNGA NA MANCHESTER CITY. Elcapitano Maestro 🗣 Sajili za enzo maresca ni wazi kuwa ana...
31/08/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

ILIMAN NDIAYE KUJIUNGA NA MANCHESTER CITY.

Elcapitano Maestro 🗣 Sajili za enzo maresca ni wazi kuwa anataka kuwania ubingwa wa ligi msimu huu 2026-27 na kutaka kufanya vizuri katika michuano ya uefa champions league.

Liverpool walimnyatia sana ndiaye lakini yeye mwenyewe (mchezaji) amechagua kwenda Man City kwa mujibu wa Fabrizio Romano.

Enzo Maresca anachagua wachezaji ambao hatahitaji maelekezo mengi katika kuwafundisha 😀.

💁🏾‍♂️

DARASA HURU 💁🏾‍♂️BRADLEY BARCOLA AMEJIUNGA NA LIVERPOOL 😀.Elcapitano Maestro 🗣 Moja ya sajili ambayo nilikuwa naisubiri ...
31/08/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

BRADLEY BARCOLA AMEJIUNGA NA LIVERPOOL 😀.

Elcapitano Maestro 🗣 Moja ya sajili ambayo nilikuwa naisubiri sana ni kuona Barcola akijiunga na Liverpool.

Hatimae Liverpool wametoa dau la €140 milioni kuinasa saini ya Barcola ambae amesaini mkataba wa miaka 5.

Kushoto Barcola katikati anamaliza Isak na kulia anazima Muñoz ni moja ya safu nzuri ya ushambuliaji.

Liverpool sasa waboreshe eneo lao la katikati la uwanja na kulifanya liwe lenye nguvu zaidi k**a misimu miwili kurudi nyuma.

Kila la kheri Andoni Iraola.

💁🏾‍♂️

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255620587262

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Elcapitano Maestro posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Elcapitano Maestro:

Shortcuts

Share

Category