25/07/2023
🕸..WATAALAMU WA SHERIA WANASEMA...
Mwanasheria wa Yanga SC Simon Patrick kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika
"Kanuni ya 62 (4) - Kanuni za Ligi Kuu, Toleo la mwaka 2022 inasema;
“Mchezaji wa kigeni anayeruhusiwa kusajiliwa kwenye Ligi Kuu ni yule anayecheza katika timu ya Taifa ya nchi yake au Ligi Kuu ya nchi husika.
Mchezaji kutoka Amerika ya kusini na Ulaya, lazima awe anacheza angalau kuanzia Ligi Daraja la Tatu (Kitaifa, kutegemea mfumo kwa nchi husika).
Mazingatio ya Daraja mchezaji analocheza kabla ya usajili wake kwenye Ligi ni kwa wakati husika au kipindi kisichozidi miezi sita tokea ameachana na timu yake ya mwisho kwa mchezaji aliye huru” Mwisho wa kunukuu..
Sasa k**a mchezaji katoka kwenye Ligi ya Mkoa au Ligi daraja la 4 huko Amerika ya kusini, usajili wake utakuaje hapa nchini? Naombeni kuelimishwa😎".