07/05/2025
KUKOPESHA WASANII WASIO NA ELIMU YA FEDHA SERIKALI IMEKOSEA- MUSUKUMA
Mbunge wa Geita Joseph Kasheku Musukuma wakati akichangia kwenye bajeti ya wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amekosoa kitendo cha serikali kupitia mfuko wa sanaa kukopesha mabilioni ya fedha wasanii ambao wengi wao wameshindwa kurejesha mikopo hiyo.
Amesema Wasanii wengi hawana elimu ya fedha, hivyo wengi wao wameitumia mikopo hiyo kununua magari ama kuoa na hivyo kujikuta wanashindwa kutimiza malengo ya mikopo waliyopewa.
Mbunge Msukuma amesema ni vyema mikopo hiyo ikatolewa kwa watayarishaji (producers) badala ya kukopesha wanaoonekana kwenye Tv (Luninga) kwa kuangalia mionekano yao (shape) kitendo kinachosababisha serikali kukosa marejesho ya mikopo hiyo.