14/02/2023
"Huo ni zaidi ya mchezo wa kawaida ambao mwanadamu amewahi kuona au kufikiria. Sisi k**a Simba tunataka jambo moja tu, ni ushindi mbele ya Raja AC”
"Kwa mujibu wa CAF, mchezo ni saa 1:00 usiku, awali tulithibitisha kucheza saa 10:00 jioni lakini ratiba ya mwisho kutolewa na CAF imekuwa saa 1:00 usiku. Tumewaandikia CAF kuwaomba muda wa mchezo uwe saa 10:00 jioni."
"Naomba kuwambia mashabiki wa Simba tuanze kujiandaa na muda wa saa 1:00 usiku. Lakini sisi hatuangalii muda, muda wowote tupo tayari kupambana ili kupata ushindi. Na k**a mnakumbuka tulishawahi kucheza saa 4 usiku na tukapata matokeo."
"Waamu*i wa mchezo wanatokea Cameroon. Kuhusu Raja AC tayari tumeshawatumia taarifa kuwauliza watafika lini Tanzania lakini hadi sasa hawajasema lini watakuja."
"Kuhusu Sadio Kanoute hatakuwepo kwenye mchezo unakuja kutokana na kuwa na kadi tatu za njano. Kuhusu Saidi Ntibazonkiza sasa ameshapona, wengine ni Peter Banda."
"Rais wa heshima wa Simba SC, Mohammed Dewji kwa mapenzi yake na klabu ya Simba, mapenzi yake na mashabiki wa Simba alituomba tupunguze viingilio. Mzunguko sasa ni Tsh. 3,000, VIP C- Tsh. 10,000, VIP B - Tsh. 20,000 na VIP A - Tsh. 30,000."
"Tumeona taarifa kutoka kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akitangaza kwamba Rais Mama Samia atanunua kila goli kwa Tsh. 5 milioni."
"Sisi k**a Simba kwanza tumefurahi, tunaichukulia k**a ni agizo, mama anatutaka tukafunge magoli. Tumepokea na Jumamosi tunamuahidi kufunga magoli mengi kadri iwezekanavyo. Wachezaji wako tayari kumfurahisha mama na kuwafurahisha Watanzania."
"Simba tunapoingia kwenye mechi hizi za kimataifa tunakuwa tumeingia kwenye msimu wa sherehe. Kesho Jumatano kuanzia majira ya saa 5 asubuhi tutafanya u*indu*i bab kubwa kwenye tawi la Home Boys lililopo Tegeta.”
"Tunakwenda kwenye mechi kubwa tukijiamini maana tunaamini tunachokwenda kukifanya kwenye michuano hii."
"Ili tuweze kupata matokeo Jumamosi basi mashabiki wa Simba 60,000 tuwaone pale Kwa Mkapa. Wakijaa mashabiki wa Simba hakuna timu Afrika hii inaweza kutoka salama. Tayari tumeanza kuuza tiketi, nunua tiketi yako mapema."- Ahmed Ally.