02/09/2026
MZIZE NA DICKSON JOB WABAKIA JOHANNESBURG KWA AJILI YA VIPIMO
Nyota wa Yanga SC, Clement Mzize na Dickson Job, wameondoka Dar es Salaam pamoja na msafara wa timu kuelekea Botswana, lakini safari yao imeishia kwa muda Johannesburg, Afrika Kusini.
Wawili hao wamebaki kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya katika hospitali walikofanyiwa upasuaji awali.
Kwa mujibu wa Ali Kamwe, hakuna haraka ya kuwarejesha uwanjani hadi majibu ya vipimo yatakapothibitisha kuwa wako tayari kurejea kwenye ushindani.
Wakati huo huo, timu ya Yanga SC tayari imewasili salama nchini Botswana kwa ajili ya mchezo dhidi ya Gaborone United utakaopigwa Jumamosi, Septemba 5, saa 2:00 usiku kwa saa za Tanzania.