31/05/2025
๐จGUINEA IMEKATA RUFAA TENA DHIDI YA TANZANIA KUFUZU AFCON.
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) litafanya kikao cha kusikiliza rufaa inayohusu Timu ya Taifa ya Guinea ๐ฌ๐ณ na Taifa Stars ๐น๐ฟ mnamo Juni 11 saa 5:00 asubuhi.
Kikao hicho kitafanyika katika makao makuu ya CAF yaliyopo Nchini Misri ๐ช๐ฌ Cairo.
Fahamu hili: Guinea inapanga kuandaa ujumbe wa watu 20 kwenda Misri kukutana na Kamati ya Rufaa ya CAF.
Ikumbukwe kuwa : Guinea wanadai kuwa Tanzania ilimchezesha mchezaji ambaye hakutambulika na ambaye namba ya jezi yake haikuwa kwenye orodha ya wachezaji wa siku ya mechi, katika mchezo uliochezwa tarehe 19 Novemba 2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kesi ya awali ya Guinea ilikataliwa, lakini wamekata rufaa, na CAF imepanga kusikiliza hoja zao tarehe 11 Juni.
Source : Micky Jr