28/08/2026
DOUMBIA ATAFUNGA TU - BARKER
TAARIFA ZOTE MPYA ZA SIMBA UTAZIPATA NDANI YA GROUP KUBWA LA SIMBA WHATSAPP TUMA NENO NIUNGE SIMBA KWENDA WHATSAPP NAMBA
0763999638
0763999638
Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amesema mshambuliaji Ibrahim Doumbia alikosa bahati ya kuweka mpira kambani kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union lakini ana imani mshambuliaji huyo atafunga mabao mengi.
Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ambao Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0, Doumbia alipata nafasi kadhaa ambazo alishindwa kutumia licha ya kukaribia kufunga.
"Doumbia ni mshambuliaji mzuri, sisi tuna muamini, nafikiri leo alikosa bahati tu ya kufunga lakini amefanya jitihada kubwa uwanjani"
"Hii ni hali ya kawaida kwa mchezaji mgeni, anahitaji kuzoea mazingira pamoja na mfumo wetu wa uchezaji kwa ujumla"
"Sina wasiwasi nae, ni mchezaji mzuri naamini atatufungia mabao mengi msimu huu," alisema Barker.
Mashabiki wa Simba wameaswa kuendelea kumuunga mkono mshambuliaji huyo ili wampunguzie presha ya nje ya uwanja ili aweze kufanya vyema.
SIMBA TAARIFA GROUP BORA LA WHATSAPP CHIMBO LA HABARI ADMIN MKUU WHATSAPP NAMBA
0763999638
0763999638