25/05/2026
📌 PROFESSIONAL ATHLETE PROFILE – MARTHA MABULA (MARTHAFIT)
Martha Mabula, anayejulikana k**a Marthafit, ni mmoja wa wanamichezo wanaoongoza katika kizazi kipya cha female bodybuilding & fitness nchini Tanzania. Akiwa na msingi wa nidhamu, mazoezi ya kiwango cha juu na falsafa ya kuendeleza afya ya mwili kwa wanawake, Martha ameendelea kujijengea nafasi imara kwenye majukwaa ya kitaifa na kikanda.
ameanza safari yake ya bodybuilding mwaka 2019 na tangu wakati huo ameshiriki na kung’ara katika mashindano mbalimbali, ikiwemo:
Miss Bikini East Africa – Mshindi mara 2
Miss Fitness Tanzania – Nafasi ya Pili
Mr. Tanzania-2019
Mr. 001- 2021
Mr. Kamkunji - 2023
Mr. East Africa-2023
Mr. East Africa-2024
NPC African Qualifier-2025
Mbali na ushindani, Martha anajulikana kwa dhamira yake ya kipekee ya kukuza mchezo wa bodybuilding kwa wanawake, kupitia elimu, uhamasishaji na mfano wa kuigwa katika maisha ya mazoezi. Anaamini katika nguvu ya wanawake kujenga miili yenye afya, kujiamini na kushindana bila hofu.
Nje ya jukwaa la mashindano, Martha hupendelea kusoma vitabu na kuendeleza fitness lifestyle inayompa uwiano kati ya mwili, akili na malengo yake ya muda mrefu.
Kwa sasa, Martha anajiandaa kupanda viwango zaidi katika mashindano ya Afrika na kimataifa, huku akibaki kuwa sauti muhimu katika kuhamasisha wanawake kuingia kwenye mchezo huu kwa ujasiri na maarifa.