14/06/2026
Real Madrid CF inaripotiwa kufikia makubaliano ya kumsajili beki wa kushoto wa Hispania, Marc Cucurella, kutoka Chelsea FC katika dili linalotajwa kuwa na thamani ya zaidi ya euro milioni 50.Kwa mujibu wa taarifa hizo, Cucurella tayari ameridhia kujiunga na miamba hiyo ya La Liga na yupo tayari kuanza safari mpya ya soka ndani ya Uwanja wa Santiago Bernabéu.
Iwapo dili hilo litakamilika rasmi, Real Madrid itaendelea kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kuongeza beki ambaye ameonyesha kiwango bora katika misimu ya hivi karibuni kupitia uwezo wake wa kushambulia, nidhamu ya ulinzi pamoja na nguvu ya kucheza katika mfumo wa kisasa wa mabeki wa pembeni.Usajili huo unaweza kuwa sehemu ya mpango wa Real Madrid kuendelea kujenga kikosi chenye ushindani mkubwa kuelekea misimu ijayo.