12/05/2025
“Ni vyema kila mtu akafahamu kwamba Simba ni mwana fainali ya CAF, fainali ya mara ya pili baada ya ile ya mwaka 1993 na safari hii tukicheza na RS Berkane ya Morocco.”
“Katika kufika fainali hii tunayo kila sababu kumshukuru Rais na Mwenyekiti wa Bodi, Mohammed Dewji. Amefanya kazi kubwa sana, amepambana na amepigana vita kubwa kuhakikisha Simba inafika fainali ya Kombe la Shirikisho.
Mo Dewji amefanya kila kinachowezekana ndani ya klabu yetu. Sisi Wanasimba hatuna budi kumshukuru, kumpongeza na kumuombea aendelee kupambana kuiba Simba ubingwa wa Afrika. Tumuombee kwa Mwenyezi Mungu ampe afya njema, kuimarisha uchumi wake na kuendeleza mapenzi yake kwa Simba Sports Club.”
“Lakini hatuna budi pia kumpongeza Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu ya kufika fainali ya Afrika. msimu huu amejitoa sana, amepambana sana, amekuwa bega kwa bega na Simba, ameilea Simba k**a mtoto wake wa kumzaa mwenyewe, amekuwa akiisimamia Simba kwa kila hatua na leo Simba inakwenda kucheza fainali ya Afrika. Yeye kwa kushirikiana na wajumbe wa bodi wamefanya kazi kubwa. Wapo wengi wamepambana lakini hawa ndio machampioni wetu wa kuifikisha Simba hapa tulipofika.”
“Baada ya kumalizana na Berkane, Mnyama atarudi nyumbani kwa mchezo wa marudiano na kombe litakuwepo Uwanja wa Mkapa. Kuelekea mechi zetu za fainali tunakwenda na kauli mbiu ya TUNABEBA. Tunamaanisha ubingwa wa Afrika safari hii tunabeba. Kuanzia sasa kila Mwanasimba aiweke moyoni hiyo na aanze kufanyia kazi kuhakikisha kombe hili tunabeba.”- Semaji Ahmed Ally.