12/03/2026
John na Happiness walikuwa wapenzi wa dhati kijijini kwao baada ya wote wawili kufeli mtihani wa darasa la saba.
John alikuwa na ndoto za kawaida za kijijini; alipanga kulima mashamba, kuchoma mkaa, na kujenga nyumba ndogo ili waweze kuishi pamoja na kulea watoto wao.
Hata hivyo, Happiness alikuwa na ndoto tofauti kabisa, kwani moyo wake ulitamani maisha ya mjini na anasa zake. Fursa ilipojitokeza kwa Happiness kwenda Dar es Salaam kufanya kazi za ndani, John alipatwa na hofu kubwa ya kumpoteza mpenzi wake.
Katika hali ya kukata tamaa, alijaribu mbinu ya kutaka kumpa Happiness mimba kabla hajaondoka ili "amfunge" asisahau kwao, lakini Happiness alikuwa mwerevu na alikwepa mtego huo kwa kukataa kukutana naye usiku wa safari yake.
Baada ya Happiness kuondoka na kufika Dar es Salaam, John alijitahidi kwa kila hali kuendeleza mawasiliano yao ili kulinda penzi lake.
Changamoto ilikuwa simu ya John ambayo betri yake ilikuwa mbovu na haikai na chaji kabisa. Kwa sababu alitaka kuongea na Happiness kila wakati, John alifanya jambo lililowaacha watu wengi na mshangao: alianza kutembea na jenereta dogo begani na mkononi akiliwasha na kuchomeka chaja ya simu yake popote alipoenda. Alikuwa ananunua petroli kila siku ili tu asikose nafasi ya kuchati na mpenzi wake, akiamini kuwa juhudi hizo zitamfanya Happiness aone thamani ya upendo wake hata akiwa mbali.
Hata hivyo, Happiness alipoanza kuonja maisha ya jiji, mambo yalianza kubadilika. Alianza kupata vyakula vitamu k**a chipsi, kupelekwa matembezi ya beach, na kuona maisha mapya ambayo yalimfanya ayaone maisha ya kijijini na John k**a mzigo.
Ili kujiondoa kwenye usumbufu wa John, Happiness aliamua kubadilisha namba ya simu na kukata mawasiliano kabisa. Habari hiyo ilimvunja moyo John kiasi cha kumfanya achanganyikiwe na kujaribu kujinyonga nyuma ya nyumba yao.
Kwa bahati aliokolewa, lakini viongozi wa mtaa walimpa adhabu ya viboko kwa kitendo hicho, jambo lililomfanya aone aibu na kuamua naye kukimbilia Dar es Salaam.
Maisha ya John jijini Dar es Salaam hayakuwa na dira k**a alivyotarajia mwanzo. Badala ya kumtafuta Happiness au kuanza maisha ya maendeleo alimkosa kwani hakuwa na mawasiliano naye, John alianza kazi ya kuosha magari na kutumia mapato yake kwenye starehe za pabu.
Alianza kuwa mtu wa wanawake wanaojiuza buku tatu Kila siku alitenga bajeti ya elfu tatu hali hiyo ilifanya asahau kabisa ndoto zake za kilimo na familia.
Leo hii, John amemsahau kabisa Happiness, lakini amekuwa mtu wa ajabu aliyepoteza mwelekeo wa maisha.
Ni kipi unajifunza hapa?