06/10/2020
OCTOBA 18 YANGA ANA NAFASI ILA AFANYE HAYA
Mara ya mwisho kukutana hapo Matokeo yake yalishangaza sana, Yanga alipigwa bila huruma Goli nne kwa Moja, Yani alipigwa Nne na Akapigiwa Pira Sambusa.
Matokeo ya Mechi ijayo kiukweli anayo Mungu tu ila Sisi mashabiki tunakuwaga na uwezo wa Kuhisi tu Matokeo kutokana na Mwenendo wa Hizi timu.
Kikuweli ile Yanga iliyopigwa Nne sio hii ya msimu huu hata kidogo lakini pia ile Simba iliyopiga nne sio hii kabisa japo haijaongezeka sana.
Mechi ijayo Heshima pekee ambayo Yanga wanaisaka sasa ni kushinda huu mchezo ili kufuta ile Nne tunayoikumbuka,
Ili Yanga ashinde huu mchezo lazima kwanza afanye Yafuatayo
1. Aingie uwanjani kucheza mpira sio kulipiza kisasi.yani asiingie kwa lengo la kulipa aingie kusakata Soka safi na kutafuta Magoli
2. Ulinzi imara, kiukweli katika timu ambazo hautakiwi kuzishambulia kizembe ni Simba wana uwezo mkubwa sana wa kusak**a lango lako hasa beki zako zikiwa Zimetoka
3. Yanga wahakikishe wanaingia uwanjani wakiwa hawana makando kando nje ya uwanja (sjui mnaelewa) yani wahakikishe timu nzima inaingia na akili moja sio huyu anawaza mkataba huyu anawaza mshahara hajapewa. Watapigwa tena.
4. Hata k**a Morrison ataanza ila Yanga wasimuwaze kabisa wala wasihangaike naye, maana wanaweza kuingia wakiwaza kumkaba ili aaibike wakasahau Simba kila mtu anajua kufunga waingie na mpango wa kuizuia timu nzima.
5. Yanga mpaka sasa hawana kocha (kosa kubwa sana) Yanga ili wawe sawa wampe majukumu Mwalimu Mwambusi kwenye huo mchezo ila wakitaka kumvuruga wamletee kocha hapa katikati kabla ya Octoba 18, wataivuruga timu Kocha mpya aje baada ya hii mechi.
6. Yanga waepuke kutoa dau kwenye huu mchezo yani yale mambo ya mkishinda mnapata million kadhaa, sjui kila anayefunga anapewa million kadhaa yatawavuruga sana maana kila mchezaji anaitaka hela hawatacheza kitimu.
7. Mwisho kabisa Yanga anahitaji Kuingia na mbinu zake za siku zote ila wasije wakajaribu kuiga zile biriani za simba, zile wamezifanyia mazoezi Miaka sita nyuma ndio wanazifanya sasa.
ALL IN ALL CHAMA NA KONDE BOY MPAKA SASA NI WAZIMA WA AFYA