15/11/2023
YANGA INAENDA KWENYE NJIA SAHIHI KISOKA
Siku zote njia ya mafanikio Huwa ni ndefu na ngumu sana pia yenye shida na tabu nyingi sana ila k**a wasemavyo waswahili kuwa penye nia hapakosi njia, ndilo neno sahihi au msemo sahihi unaoweza kuutumia kuelezea njia inayopitia klabu ya Yanga Kwa sasa
Utawala wa soka wa Simba wa miaka minne mfululizo na mafanikio ya Simba kimataifa kuliwaamsha Yanga usingizini taabu na mahangaiko ya kutegemea mtu kuendesha mambo kuliwatokea puani pale mfadhili mkuu wao mfanyabiashara YUSUPH MANJI alipowachunia na kuwanyamazia ghafla bin vuu msimu wa 2016/2017 asiseme lolote huku na yeye akikabiliwa na masahibu ya utawala wa serikali ya awamu ya 5 chini rais DKT JOHN POMBE MAGUFULI.
°° Yanga walianzisha mchakato wa mabadiliko ya kiuongozi na utawala, hapa Yanga kupitia mfadhili wao GSM ambaye aliamua kuvunja kibubu na kuwaleta LA LIGA kuwapa mafunzo maalumu ya namna ya kuendesha soka kisasa... Watani zao Simba WALIBEZA NA KUKEJELI
°° Yanga wakati wakisubili mchakato wao wa mabadiliko ya kiuongozi na utawala waliamua kuajiri watu wenye ueledi mkubwa wa soka la kisasa wakamleta SENZO MBASA MAZINGISA kuwa afisa Mtendaji mkuu wao CEO akitokea Kwa mtani wao simba... Watani zao Simba WALIBEZA NA KUKEJELI
°° Yanga wakaanza kuimarisha benchi lao la ufundi na kumleta kocha NABI pia kusajiri wachezaji tofauti tofauti wa kubahatisha, ambao baadhi walifeli vibaya, lakini hawakukata tamaa na kuamua Sasa kubadili gia na kuajiri watu wenye ueledi mkubwa wa kufanya scouting ya wachezaji na kuacha ubahili wakaanza kuhusishwa na majina makubwa ya wachezaji Afrika k**a vile kina DJUMA SHABAN, FISTON KALALA MAYELE, TUISILA KISINDA, AZIZ KI... Watani zao Simba WALIBEZA NA KUKEJELI
°° Yanga wakaanza mchakato wa kutambua na kusajiri wanachama wao kidigitali pia kuwashirikisha katika matukio muhimu k**a kufanya gwaride kubwa kushangilia ubingwa, kusafiri na timu nje ya nchi, na hivi karibuni kuwaalika mashabiki na wapenzi wa klabu Yao kula supu Kwa pamoja... Wa