09/04/2026
Madrid vs Bayern analysis (1st leg)
Tuanze na idea ya Bayern kwenye ujenzi wa mashambulizi (build up) kutokea chini. Bayern wamekuwa wanawasogeza juu baadhi ya wachezaji (full backs) ambao wataenda kucheza kwenye maeneo ambayo yatampa maswali magumu mpinzani wake.
Mfano: Stanisic na Laimer wanasogea juu kwenye half spaces halafu Olise na Diaz wanatanua mapana ya uwanja. Bayern walikuwa wanafaidika vipi na muundo huu wa kusogeza walinzi wake wote wawili juu?
Kwakuwa Madrid kipindi cha kwanza walikuwa wanazuia na 4-4-2 ilikuwa na madhaifu kwa Mbape na Vin ambae kazi yao ilikuwa kusubiri mipira ya counter na kushindwa kuisaidia Madrid OOP. Turudi kwenye mada
Laimer na Stanisic wakisogea juu inawafanya Valverde na Guler wafuate mikimbio ya hao wachezaji wa Bayern, kwakuwa Laimer na Stanisic walikuwa wanaingia ndani maana yake Diaz na Olise wanaachwa kwenye situation za 1v1 dhidi ya Trent na Carreras.
Na hapo ndio tatizo kubwa lilikuwa linaanzia kwa upande wa Madrid hata ukiangalia upande wa Olise alikuwa anapita sana sababu ya 1v1 dhidi ya Carreras ambae hakuwa na game nzuri dhidi ya Bayern.
Nini walifanya Madrid kuzuia uhatari huu?
Madrid waliona njia salama ni kurudi kwenye low block ya 4-4-2 kuwaacha Vin na Mbape juu hawafu wachezaji wengine nane wazuie kwa ukaribu sana na kufunga nafasi yoyote ile katikati ya mstari. Hii ilisaidia kwa kiasi chake maana wachezaji k**a Olise na Diaz wanahitaji sana soace ili wakufunge.
Hapa wakawaacha Bayern wazunguke na mpira juu ya combact block yao ambayo waliweka huku wakisubiri nyakati za kufanya counter attacks. Kuna walikuwa wanafanikiwa kuishinda rest defense ya Bayern Munich. How?
Rest defense ya Bayern ilikuwa 2+1 (Upamecano na Tah halafu juu yao anakuwepo Kimmich) Kimmich kazi yake ilikuwa ni kuvunja aina yoyote ya pasi ambayo itatupwa kwa Mbape na Vin, k**a ikitokea akawa nyuma ya mchezo maana yake hakuna mchezaji wa kuwaokoa dhidi ya Vin na Mbape.
Mbape na Vin waliona kuna ugumu kupitia katikati mwa kiwanja maana Kimmich angekuwa rahisi kwenda kuziba mapengo ya Tah au Upamecano, sasa wao wakaamua kwenda wide ili hata Kimmich akienda kuziba nafasi speed yake ni ndogo kulinganisha na Mbape au Vin.
Licha ya hayo yote ila Vincent alikuja na moja kati ya muundo bora sana wa kufanya counter pressing.
Hii aina ya pressing hawakuwa wanafanya tu sehemu moja ila kila mchezajikwenye kila eneo alikuwa anaenda kupress pale anapopoteza mpira. Najua ni hatari sana ila risk ambayo alichukua ndio imewafanya kuwa hapa walipo.
Kuanzia namna ambavyo Madrid walipokuwa wafanya build up Kimmich unamuona amesogea juu kabisa lengo likiwa ni kuweka presha ila kuna muda kutoka kwa Kimmich kwenye kungo kulileta shida kwa Pavlovic ambae alikuwa anabaki k**a single 6 dhidi ya wachezaji wawili wa Madrid.
Bado tena unawaona Madrid ili kuua kabisa uchezaji wa Bayern ule wa wachezaji kuzunguka uwanja mzima walikuwa wanashuka hadi kwenye muundo wa 5-3-2 ili Valverde amsaide Trent kuzuia. Mambo yalikuwa mengi ila acha tusubiri tuone second leg.