28/08/2026
*STATEMENT YA MWANAHABARI NA FORMER FOOTBALLER WA TOYOYO - KWA WAKAAZI WA ZIWANI*
Mimi ni mkaazi wa Ziwani na mwanahabari ambaye nimechezea Camp Toyoyo, Jericho.
Nimeona maendeleo na vita ya Toyoyo.
Toyoyo ilijengwa na turf na Mheshimiwa Bernard Mutura - mzaliwa wa Bahati aliyecheza hapo mguu tupu. Ilikua mega project kwetu. Ilihost KPL, World Cup Trophy Tour, Chapa Dimba, na Wazee Premier League.
Lakini baadaye, kulingana na treasurer wa uwanja (iko on record), Mheshimiwa George Aladwa - mbunge wa sasa - anadaiwa kupokea Shilingi Milioni 1 kutoka kwa uwanja eti ni kulipa deni la ujenzi. Kwa sheria za CDF, hakuna kulipa deni kwa pesa za CDF. Hizi ni allegations ambazo mpaka leo hazikujibiwa vizuri. Nilipojaribu kumuhoji, sikuweza kumpata tena.
Toyoyo ilikua inachaji 4k kwa masaa mawili, na 20k kwa mechi ya Premier League. Kwa hesabu ya mtaa, hiyo ni karibu 800k kwa mwezi. Lakini Jericho All Stars na youth team ya Raul na Swaleh hawakupata chochote.
*Funzo kwa Ziwani:*
Sisi wa Ziwani tumepewa habari na kiongozi wetu wa nyumba kumi kuwa kuna allocation ya kumaliza Ziwani Ground, wakati huo huo ground haikufungwa na ili-host Kothbiro mbele yetu sote.
Mimi sisemi ni wizi. Nasema ni allegations tunazopewa k**a wakaazi, na tunahitaji majibu.
Kabla hatujaweka turf Ziwani, tuulize maswali ambayo Jericho haikuuliza mapema:
1. Pesa ya uwanja itasimamiwa na nani?
2. Revenue ikija, community team itapata nini?
3. Mtaa utapata masaa mangapi bure?
Maendeleo bila uwazi, ni vita tu.
*Mkaazi wa Ziwani, Mwanahabari wa zamani wa Camp Toyoyo