22/02/2019
Chelsea imepigwa marufuku na FIFA kutosajili wachezaji kwa madirisha mawili yajayo ya uhamisho hii ni baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka sheria na kanuni za kuwasajili wachezaji makinda.
Pia kilabu hiyo imepigwa rungu la faini ya pauni 460,000, nacho chama cha soka nchini Uingerezwa hakijaachwa salama kwani wamepigwa faini ya £390,000.
Kichocheo kikubwa kwa makosa haya nikutokana na jinsi walivyomsajili Bertrand Traore mwaka 2013.
Chelsea wana siku 90 kujitakasa kutoka kwa marufuku hiyo.
Picha kwa hisani.