07/06/2024
Jina : MOSES MBAU GITAU
Alias: MUSA/mzoefu
NAFASI: Kiungo mchezeshaji
Akiwa amezaliwa Limuru katika mojawapo ya maeneo yenye baridi kali sana nchini zaidi ya miongo mitatu iliyopita , MUSA , jina ambalo alipewa na mkufunzi wake mpya likiwa lina ukaribu sana na la Musa yule wa maandiko matakatifu aliyetwikwa jukumu la kuwaongoza wana wa Israel toka utumwani MISRI. Amekwisha valia u*i wa Limuru BATA FC, GREEN barrets na KARIRANA Fc,......Mzazi mwenye wana wawili na mmiliki wa stashahada ya uhandisi kutoka chuo anuai cha Nairobi. Kando na kuleta burudani uwanjani pia ni mfanyabiashara na mwajiriwa mchapakazi pale RUIRU.
Jina MUSA Moses Deh Frontier sio geni maskioni pa wapenzi wa soka katika Gatu*i hili la Kiambu. Sura yake ni chukizo kubwa machoni mwa magolkipa ambao wamekumbana na mashuti ya mwamba huyu akiwa anavalia u*i wa FC ALLSTARS NYACABA. Simulizi ya karne mbili zijazo haitaacha kumtaja Moses Gitau.Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa jina lake limetajwa sana na wapenzi na wafidhina wa mpira wa miguu Witeithie . Amewaheshimisha wakazi wa NYACABA na kutetea hadhi yao kwa damu, nyama na mifupa . A real soldier! Alijiunga na makachinja wa ALLSTARS akitokea ku*itesa nyasi kule Karirana mwaka wa 2022 na baada ya kipindi kifupi cha mazoezi alimridhisha mwalimu mkuu Mwadhamu Bonnie na moja kwa moja akatia wino kandarasi iliyomrasimisha kuwa mali ya ALLSTARS.
Ndani ya msimu wake wa kwanza kwenye timu hii alikuwa miongoni mwa kile kikosi cha The Invicibles ambao walipiga msimu mzima wa subcounty league pasi kupoteza mechi yoyote na kupanda daraja la ligi ya kaunti. Ni kiungo mwenye uhusiano mzuri sana na nyavu. Mguu wake wa kulia unampa jina zuri kwa uwezo wa kupiga makombora yenye madhara makubwa sana kwa timu pinzani .Mwili jumba kimuonekano ila ni mpambanaji mwenye mapafu ya duma pale uwanjani. "MTUNGI MIA MIA"
Ufanisi huu uwanjani na pia uongozi mazoezini ulimshawishi mkufunzi kumvisha kitambaa cha unahodha ndani ya msimu mpya wa mwaka 2022 sambamba na 2023. Hii ilikuwa chachu ya ufanisi mkubwa na maku*i ambayo ameyapata k**a mchezaji. Hadi sasa akiwa kiungo aliyecheka na nyavu mara nyingi sana katika wodi nzima ya witeithie ,nitamuita catalyst yaani kichocheo kikubwa cha kuifanya timu icheze . Fundi mwenye viegezo vyote vya kuwa fundi.
Akiwa kiungo anayecheza eneo ambalo linatoa uwamu*i mkubwa wa kufanya timu icheze,,ana uwezo wa kukaa na mali mguuni,kupita kwenye pori la wapinzani na kubuni mabao mengi. Bongo zangu zina kumbukumbu ya mabao yake mawili dhidi ya Youngstars pale nyumbani FLATS ARENA. Yote mawili yakiwa hakikisho ya ufundi wake wa kupiga mipira mifu. "dead ball specialist."Tutakuenzi k**a linavyoenziwa jezi nambari kumi kule Rio de Janeiro na Sao Paulo Brazil ,Taifa la pekee lenye mataji matano ya kombe la dunia. Kwenye mahojiano ya kipekee hivi maju*i kaniibia siri anapania kuwa mwalimu wa soka pindi baada ya kustaafu kutoka uwanjani.
Musa mola akujalie miaka mingi ya kucheza soka na kuleta burudani,kuwa kielelezo kwa yule kijana mdogo mwenye ndoto ya kucheza mchezo huu wenye ufuasi mkuu sana duniani. Asante sana mwalimu MERCY kwa kutuachia mumeo atupe burudani uwanjani
# COYA