08/07/2022
Jumapili hii ya tarehe 10/07/2022 tumealikwa kwenye kinyang'anyiro cha mchezo wa kambumbu # Wapopa Soccer Cup. Hii ni awamu ya tano ya shindano hili ambalo lilizinduliwa Agosti 2020.
Tuliwaelezea hapo awali kuwa vilabu zote kutoka wadi ya South Bukusu zitaungana kulingana na maeneo ambako zinatoka ili tupate timu nne za kushiriki.
Baada ya kuungana tutatumia majina haya kwenye usajili.
1. Tabuti FC.
2. Kibachenje FC.
3. Kimatuni United.
4. Lumboka FC.
Kulingana na mdhamini wa mitanange hizi bwana Silas Wapopa, timu zote nne zitapata zawadi k**a ilivyo desturi.
ZAWADI.
1. Ksh. 20,000
2. Ksh. 10,000
3. Ksh. 7,000
4. Ksh. 5,000
Tunaomba timu zote zianze kujiandaa vyema na tuzingatie sheria za shirikisho la soka duniani siku ya mchezo. Kila mmoja anapaswa kufika kwenye uwanja saa moja unusu asubuhi.
Mashindano haya yameratibiwa kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Lumboka.
Ikiwa kuna mwanasiasa yeyote angependa kuwa nasi siku hiyo aje auze sera zake kwa njia inayostahili na tudumishe amani tusilete vurugu zozote.
Tunaomba wakaaji wote wa South Bukusu watokezee siku hiyo kwa madhumuni ya kushangilia timu zao.
Kufikia hapo sina la ziada ila kukutakia wikiendi bomba mbeleni. Tusambaze ujumbe!!
# Wapopa Cup!
# 5th Edition!
# South Bukusu Ward!
# Khupa khucheee!!!